Rc mndeme awaomba akina mama kusimamia suala la lishe na ukatili kwa watoto, changamoto ya umeme kuisha mkoani shinyanga

Na
Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewaomba akina mama Mkoa wa
Shinyanga kusimamia vyema suala la lishe kwa watoto ili kumaliza tatizo la
udumavu.

Ameyasema
hayo wakati akizungumza na jumuiya ya wanawake wa kiislam Mkoa wa Shinyanga
(JUWAKITA) ambapo pamoja na mambo mengine amesema Mkoa wa Shinyanga mpaka sasa
una asilimia 27.5 ya tatizo la udumavu.

Rc
Mndeme amewaomba akina mama kuwa  mstari
wa mbele kusimamia suala la upatikanaji wa lishe bora kwa watoto ili kuondoa
tatizo la udumavu kwa watoto.

“Akina mama sisi ni wajibu wetu kusimamia kuhakikisha
kwamba watoto wetu hasa walio na umri chini ya miaka mitano wanapata lishe bora
na tuondokane kabisa kutoka asilimia 27.5 tufike asilimia 0 linawezekana mtoto
chini ya miaka mitano ale chakula ambacho kinafaa tuondokane na kuwalisha
watoto chakula kwa mazoea kwa sababu sisi akina mama ni wasimamizi wakubwa wa
makuzi katika familia zetu tusimamie suala la lishe kwa watoto wetu ili udumavu
ndani ya Mkoa wetu uondoke bahati nzuri Mkoa wetu una kila aina ya chakula
hatuna sababu ya kuendelea kuwa na udumavu katika Mkoa wa Shinyanga akina mama
wenzagu naomba tumuunge mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan masuala ya
lishe tuyasimamie”.
amesema RC Mndeme

RC
Mndeme amewaomba wanawake katika Mkoa wa Shinyanga kuendelea kukemea mmomonyoko
wa maadili ikiwa ni pamoja na kutokomeza ukatili unaoendelea kufanyika kwenye
familia ikiwemo vitendo vya ubakaji na ulawiti.

“Tukemee suala la mmomonyoko wa maadili miongoni mwa
jamii yetu tukemee vitendo vya ubakaji na ulawiti lakini tuna kila sababu ya
kuyaongea haya kuanzia ngazi ya familia, tuongee na familia zetu utandawazi
unakua tuyaige yale mazuri yasiyofaa tuachane nayo lakini tumwambie mtoto
kwamba hilo eneo ni eneo lako hakuna mtu mwingine mwenye ruhusa ya kupashika
tuendelee kuwafunda watoto wetu kuanzia wakiwa watoto mpaka wakubwa wakatae
ukatili lakini tuwaambie watoto wetu wasitamani utajiri wa haraka haraka Nyumba
Gari tafuta kipato kilicho halali haya matendo ya ubakaji ulawiti ni chukizo
mbele za mwenyezi Mungu”.
amesema RC Mndeme

Katika
hatua nyingine RC Mndeme ameelezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha
Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo amesema kwa muda mfupi
Rais Dkt. Samia ameleta fedha takribani tirioni moja kwa ajili ya utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya
pamoja na miundombinu Mkoani Shinyanga.

Aidha
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameeleza kuwa Rais Dkt. Samia
tayari ametoa fedha zaidi ya Bilioni 275 ambazo zitatekeleza mradi wa kuzalisha
umeme kwa njia ya jua katika Wilaya ya Kishapu ambapo amesema hatua hiyo
itasaidia kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme Mkoani Shinyanga.

Baadhi
ya viongozi wa jumuiya wa wanawake wa kiislam Mkoa wa Shinyanga (JUWAKITA)
waliohudhuria hafla hiyo wamesema wataendelea kushirikiana na serikali ikiwemo kupambana
na ukatili na uhalifu ambao unachangia kurudisha  nyuma maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amekutana na kuzungumza na wanawake
wa jumuiya ya kiislam Mkoa wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine
wamejadili kuhusu maendeleo huku akipokea changamoto zilizopo Mkoani Shinyanga
na kwamba ameahidi kuchukua hatua kwa watu wanaokwenda kinyume na taratibu za
Nchi.

Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza katika hafla hiyo ambayo
amekutana na jumuiya ya wanawake wa kiislam Mkoa wa Shinyanga (JUWAKITA) kuzungumzia
maendeleo ya Mkoa huo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya
wanawake wa kiislamu Mkoa wa Shinyanga
(JUWAKITA)
 Bi. Aisha
Juma akizungumza kwenye hafla hiyo.