Rc tanga na tan trade kushirikiana uhamasishaji wenye viwanda kushiriki maonyesho ya viwanda

 

Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kumalizika mkutano wa wadau wa viwanda mkoani Tanga kulia
ni
Naibu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Latifa Mohamed Khamisi
NAIBU
Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Latifa Mohamed
Khamisi akizungumza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
AFISA wa  Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga Gibson George  akizungumza wakati wa mkutano huo
MKURUGENZI Mkazi wa Kampuni ya Simba Cement Mhandisi Benedict Lema akichangia jambo kwenye  mkutano huo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu wadau wa mkutano huo wakifuatilia matukio mbalimbali
SEHEMU ya Wadau wa Viwanda mkoani Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali

 

NAIBU Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Latifa Mohamed Khamisi
amesema kwamba watashirikiana kwa ukaribu na wenye viwanda mkoani Tanga kuhakikisha
wanafanikiwa na kuendelea kukua kibiashara.

Latifa aliyasema hayo
leo wakati wa mkutano wake na wadau wa viwanda Mkoani Tanga uliofanyika kwenye
ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo wamefika mkoani Tanga kuona namna ya kutatua
changamoto za wenye viwanda hatimaye viweze kuzalisha na kuuza kwenye masoko
kama ilivyokuwa miaka ya nyuma

Alisema hilo
litasaidia kwa asilimia kubwa kurudisha enzi za miaka ya nyuma ambako kulikuwa
na masoko mpaka ya ukanda wa afrika masharika pamoja na masoko ya ndani ili
kuwawezesha kuweza kunufaika kupitia viwanda hivyo.

“Leo tumefika mkoani
Tanga kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella tunatoa
shukrani kwa kutupokea na kukubali agizo la Rais la Tanzania ya Viwanda”Alisema

 Alisema kwamba mkoa huo unawaunga mkono kwenye
maandalizi ya maonyesho makubwa ya kitaifa ya viwanda vya Tanzania kwa kushirikiana
na mkoa kuhamasisha viwanda vya Tanga kuweza kushiriki.

“Kama unavyofahamu
Tanga kulikuwa na historia kubwa ya viwanda ambavyo vilikuwa vinauza bidhaa
kwenye ukanda wa Afrika vilikuwa vinatoka Tanga lengo la RC ni kuhakikisha
viwanda hivyo vinafufuka na ndio maana tupo hapa kwa kushirikiana na mkoa tumefika
kuhamasisha ushiriki wa maonyesho ya Tano ya viwanda vya Tanzania”Alisema

Alisema kwamba
maonyesho hayo ni fursa adimu kwa viwanda ikiwemo kujifunza na kujua mashine na
kuwakutanisha wazalishaji wa mali ghafi na wenye viwanda wenyewe kutatua
changamoto za maendeleo ya viwanda.

Awali akizungumza
katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alimshukuru Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade kwa kuandaa mkutano huo wa wamiliki na wazalishaji
katika sekta ya viwanda kwenye mkoa wa Tanga.

Alisema kikao hicho
ni mahususi kuona changamoto ambazo zinawakabili lakini kuona namna nzuri
wanaweza kushiriki kwenye maonyesho ya Tan Trade yatakayoanza Desema 3-9 mwaka
huu.

Alisema kwao ni fursa
kwa wazalishaji na viwanda ikiwemo wakazi wa mkoa huo kwa sababu kadri viwanda
vinavyozidi kupanuka kimasoko ndio uzalishaji unaongeza na unapoongeza unasaidia
uhitaji wa malighafi na wafanyakazi ili uweze kuongeza uzalishaji.

“Niwashukuru Tan
Trade kuendesha kikao hichi na kuamua kuja Tanga kwa sababu Tanga ni viwanda na
viwanda ni Tanga lakini la la pili uwepo wa maonyesho hayo ni fursa kwa
wawekezaji watatumia nafasi hiyo kujitangaza na kujifunza na kuona fursa
zinazopatikana kwenye maonyesho”Alisema

Hata hivyo alisema
wao kama mkoa watahakikisha Tantrade na wenye viwanda kuendelea kuwapa
ushirikiano ili dhamira ya Rais ya yenzi wa uchumi wa viwanda iweze kufikiwa
kwa kiwango kikubwa na kuwa na tija kubwa.