Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea wakati wa kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma. |
Anthony Ishengoma -Dodoma
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema Sekta ya Afya
Nchini inachangia vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa Nchini kwa
baadhi ya watoa huduma ya Afya kushiriki kuficha ushaidi kwa njia ya
rushwa.

Dkt. Ndugulile amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati
wa kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge kuhusu Mpango wa
Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto
(MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma ili kujenga uelewa kwa
kamati ya Bunge kuhusu mpango huo.

Dkt. Ndugulile amesema watoa huduma ya Afya
wanawajibu wanapopata zile kesi zinazohusiana na ukatili wa Kijinsia
kuhakikisha wanazingatia miiko na misingi ya taaluma zao kuhakikisha
hawawi sehemu ya kuvuruga ushaidi.

“Sisi kama Wizara tutakapobaini kwamba mtoa
huduma wa Afya yoyote atakayeshiriki katika katika kosa la kuvuruga
ushaidi kwa waanga wa ukatili wa kijinsia hapa Nchini tutamfutia lesseni
ya kufanya kazi ya kutoa huduma za Afya katika Nchi yetu’’. Aliongeza
Dkt. Ndugulile.

Pamoja na masuala ya ukatili wa Kijinsia
Dkt. Ndugulile amesema pia vijana wengi wanaanza kujamiina wakiwa katika
umri mdogo na kwa mjibu wa takwimu za masula ya ukimwi za mwaka 2017
zinaonesha asilimia 40 ya Watanzania ni vijana na kati hao mabinti peke
yake ni 80%.

Kufuatia hali hiyo ya vijana kujihusisha na
masuala ya kujiimiana Dkt. Ndugulile amesema serikali inakusudia
kupeleka Sheria Bungeni ili kupunguza umri wa vijana kuanzia miaka 15
kupima umri kwa hiari lakini pia kujipima wenyewe na kuweza kujilinda
lakini pia kulinda wenzi wao.

Aidha Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa sheria
iliyopo inasema mtoto chini ya umri wa miaka 18 harusiwi kupima virusi
kwa hiari labda kwa ruhusa ya mzazi wake lakini wiki ijayo Wizara
inapeleka bungeni mabadiliko ya sheria ili suala la kupima virusi kwa
hiari lianze kufanyika mpaka umri wa miaka 15 kwa kuwa watoto sasa
wanaanza kujiamiina katika umri huo na bila idhini ya wazazi.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Takwimu za
Viashiria vya Hali ya Afya Nchini zinaonesha kwamba kati ya 27% ya
mabinti walio katika umri wa miaka 15-19 mmoja kati ya watatu ama ni
mjazito au ana mtoto hii inatoa picha kwamba watoto hawa wanaanza ngono
katika umri mdogo ndio maana serikali inatoa chanjo ya kansa ya mlango
kizazi kwa watoto wa kike wenye umri huo lakini pia sula limepelekea
kufanyika kwa marekebisho ya sheria ili wapime virusi kwa hiari.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bw. Peter Serukamba amewataka
Wajumbe wa Kamati yake kuwa mabarozi wa masuala ya ukatili wa Kijinsia
Nchini ili masuala hayo yaweze kupewa kipaumbele katika Bajeti za Wizara
mbalimbali Serikalini.

Pamoja na maoni yake hayo Bw. Serukamba
ameyataja matendo ya ukatili kuwa yamekuwepo kwa mingi lakini Jamii kama
zilivyo mila na desturi zetu imukuwa ikifanya vitendo hivyo kwa usiri
tofauti na wenzetu wa Nchi za Magharibi ambapo watu wanajitangaza
hadharani kuwa ni wao ni mashoga na wanaweza kujitokeza hata kugombea
nafasi za juu katika uongozi.

Aidha kiongozi huyo wa Bunge ameongeza kuwa
pamoja na uwepo wa sheria mbalimbali lakini haitoshi tu kutokomeza
matendo haya hivyo kuitaka Wizara pamoja na wadau kutoa elimu ya kutosha
kwa umma ikiwemo adhabu kwa wote wanaohusika na makosa haya kupewa
adhabu kali.

Bw. Serukamba ameutaja umasikini kuwa
sababu mojawapo ya kuchochochea ukatili wa kijinsia kwa wanawake kwa
kuwa baadhi ya wanawake wanakubali kunyanyaswa kwasababu ya umasikini wa
kipato na utegemezi hivyo kukubali kupigwa au kuonewa kwa namna
mbalimbali.

Semina ya wabunge kuhusu Mpango wa Taifa wa
Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA)
imemalizika leo Jijijini Dodoma na imelenga kujenga uelewa kwa kamati
ya Bunge kuhusu masuala ya ukatili na mpanga mkakati huo wa miaka mitano
unaotegemea kukamilika mwaka 2022.