Serikali imejipanga kujenga viwanda vya mbolea nchini

Na Amiri kilagalila-Njombe

Serikali
nchini Tanzania imejipanga kuja na mpango wa ujenzi wa viwanda vya
kutengeneza mbolea nchini,ili kuondokana na tatizo la mbolea,kuwa na
mbolea zinazofaa,zenye bei naafuu pamoja na mbolea zinazokidhi mahitaji
ya udongo.

Hayo
yamebainishwa na waziri wa kilimo Mh.Japhet Hasunga mara baada ya
kukagua uwepo wa pembejeo za kilimo kwenye maghala ya wauzaji wa
Pembejeo mjini Makambako mkoani Njombe.

“Mpango
mkubwa wa kuondokana na tatizo la mbolea ili tuwe na mbolea
zinazofaa,ili tuwe na mbolea zile zinazokidhi mahitaji ya udongo
wetu,ili tuwe na mbolea zitakazokuwa na bei naafuu, mkazo tumeuweka
kuhakikisha tunajenga viwanda vya kutengeneza mbolea hapa nchini”alisema
Waziri Hasunga

Aidha
amesema mpango mwingine wa serikali kwa sasa ni kuja na bei elekezi kwa
aina zote za mbolea tofauti na sasa bei elekezi ikiwa kwa aina mbili
pekee za mbolea.

“Bei
elekezi haina mjadala,tulishatangaza bei elekezi mbolea za aina
mbili,mbolea ya kupandia DAP na UREA ina bei elekezi,bei elekezi ni bei
ya juu kabisa ambao tutawauzia mbolea kwa hiyo ina maana mawakala au
makampuni wanatakiwa kuuza chini ya bei elekezi,kuna mbolea najua
NPK,CAN,SA na zingine hazipo kwenye bei elekezi,lakini tunajipanga
vizuri ili mwakani ikiwezekana tuje na bei elekezi kwa mbolea za aina
zote”aliongeza Hasunga

Hasunga
ameiagiza taasisi ya mamlaka ya usimamizi wa mbolea ndani ya siku saba
kuhakikisha zinafikisha mbolea za aina zote hususani UREA mjini
Makambako kwa kuwa eneo hilo ni kitovu cha kilimo kwa mikoa ya kusini.

“Nimeshudia
kwamba mbolea zipo lakini hapa nimeona kuna upungufu wa UREA na sasa
hivi ndio kipindi cha kuanza kutumia UREA  kwa hiyo nimeagiza taasisi ya
mamlaka ya usimamizi wa mbolea wahakiishe mbolea inafika Makambako sio
zaidi ya siku saba”alisema tena Hasunga