Kutoka kushoto picha ya kwanza:
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju, Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima,
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole
Gabriel na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha
akimwakilisha katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii wakizungumza na
wananchi katika Kijiji cha Igunda, wilayani Mbarali na kuwasisitiza
serikali itaendelea kusimamia maslahi ya wafugaji na kuwataka wafuate
sheria na kuheshimu mipaka ya hifadhi za taifa na maeneo ya vijiji,
wakati viongozi hao walipokuwa wakihitimisha ziara ya siku mbili Mkoani
Mbeya katika Wilaya za Chunya na Mbarali kuanzia tarehe 18-19 mwezi
Novemba 2019.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akiangalia moja ya vielelezo
pamoja na kuoneshwa ramani ya mipaka iliyowekwa kutenganisha maeneo ya
vijiji na Hifadhi ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa, katika ziara ya
siku mbili Mkoani Mbeya kuanzia tarehe 18-19 mwezi Novemba 2019 akiwa na
viongozi wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya
Sheria na Katiba na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya Mhe. Albert Chalamila akiwa na makatibu wakuu kutoka Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya
Maliasili na Utalii akiwakilishwa na mkurugenzi wa idara ya wanyamapori
na Wizara ya Sheria na Katiba, mara baada ya mazungumzo kuhusu hali ya
ufugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali mkoani humo, wakiwa tayari
kutembelea maeneo ambayo yamekumbwa na migogoro ili kupata hadidu za
rejea zitakazotumiwa na wataalam ili kutatua migogoro hiyo katika ziara
ya siku mbili kuanzia tarehe 18-19 mwezi Novemba 2019.

Na. Edward Kondela
Serikali
imewataka wafugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali Mkoani Mbeya
kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na taratibu za nchi ikiwemo ya
kutoingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi za Taifa ya Ruaha na Pori la
Akiba la Ruangwa, hali ambayo imekuwa ikisababisha migogoro kati ya
wafugaji na askari wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), wanaolinda hifadhi hizo
ambapo baadhi ya migogoro hiyo imesababisha vifo vya wafugaji, askari
na mifugo.

Akizungumza
Jumanne hii (19.11.2019) wakati wa kuhitimisha ziara ya siku mbili ya
makatibu wakuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Sheria
na Katiba, waliozuru baadhi ya maeneo yenye migogoro katika wilaya hizo,
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole
Gabriel amewataka wafugaji kuacha tabia ya kuingiza mifugo katika maeneo
ya hifadhi kwa ajili ya malisho kwa kuwa ni kinyume na taratibu za
nchi.

“Serikali
inawataka wafugaji wote kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na
kutoingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi za taifa kwa kuwa ni kinyume
cha sheria pia serikali itaendelea kuhakikisha wafugaji wanafanya
shughuli zao kwa amani bila kubughudhiwa ili mradi wanafuata sheria na
taratibu za nchi ikiwemo ya kutoingiza mifugo katika mashamba ya
wakulima.” Amesema Prof. Gabriel

Akizungumza kwa
niaba ya makatibu wakuu wa wizara hizo, Prof. Gabriel amefafanua kuwa
kutokana na Tangazo la Serikali (GN) Na. 28 la Tarehe 14 mwezi Machi
mwaka 2008, ambalo liliongeza eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kutoka
Kilometa za Mraba 5,878 hadi kufikia Kilometa za Mraba 20,226 hali hiyo
imesababisha eneo la malisho kupungua kutoka hekta 259,000 za awali hadi
154,000 katika Wilaya za Chunya na Mbarali ambapo amewataka wafugaji
katika wilaya hizo kuheshimu tangazo hilo wakati serikali ikifanyia kazi
maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli ya kuainishwa kwa vijiji vilivyopo katika maeneo ya
hifadhi ili maboresho yaweze kufanyika kwa maslahi ya vijiji hivyo.

Katika ziara hiyo
ya makatibu wakuu kutoka wizara nne Mkoani Mbeya uongozi wa TANAPA
umekubali kutengeneza barabara za kuainisha mipaka ya maeneo ya hifadhi
na vijiji mara baada ya kuainishwa kwa mipaka mipya kufuatia agizo la
Rais Dkt. John Magufuli la kutambuliwa kwa maeneo ya vijiji na hifadhi
za taifa ambalo tayari linafanyiwa kazi.

Kufuatia matukio
ya mauaji ya askari mmoja wa TANAPA na askari mgambo mmoja mwaka 2018
waliouawa na wafugaji wakati wakiswaga ng’ombe waliokamatwa katika
Hifadhi ya Ruaha kuelekea Kambi ya Nyota ya TANAPA iliyopo Wilaya ya
Mbarali na tukio la hivi karibuni la Tarehe 11 Mwezi Oktoba 2019 la
kuvamiwa kwa kambi hiyo na baadhi ya wafugaji wakiwa na silaha za jadi
kwa nia ya kukomboa mifugo iliyokamatwa katika Hifadhi ya Ruaha hali
iliyosababisha kijana mmoja wa wafugaji (19) kupigwa risasi na askari wa
TANAPA na ng’ombe 14 kuuawa, Katibu Mkuu Prof. Gabriel amewataka
wafugaji kutumia njia zisizo halali kukomboa mifugo iliyokamatwa.

Akizungumza na
baadhi ya wafugaji katika Kijiji cha Igunda, Kata ya Igava Wilayani
Mbarali, katibu mkuu huyo amefafanua kwa wafugaji hao kuwa kutokana na
sheria na haki za wanyama duniani ni makosa kuua mnyama bila kuwa na
sababu za msingi hali iliyosababisha serikali kuchukua hatua kwa askari
wa TANAPA waliohusika kupiga ng’ombe hao risasi na hivyo kuwataka
wafugaji hao kuwa watulivu kwa kuwa suala hilo linashughulikiwa na
vyombo vya dola.

Aidha ameeleza
kuwa kuwa pindi mifugo inapokamatwa na askari wa TANAPA inapobainika
kuingia kwenye maeneo ya hifadhi, wamiliki wa mifugo hiyo wanapaswa
kufuata taratibu za kisheria za kulipa faini na kukabidhiwa mifugo yao
na kusisitiza kuwa ni muhimu kwa wafugaji kujiepusha kuingiza mifugo
maeneo wasiyoruhusiwa yakiwemo ya Hifadhi za Taifa.

“Sisi
viongozi wa Wizara za Mifugo na Uvuvi, Maliasili na Utalii, Mambo ya
Ndani ya Nchi na Sheria na Katiba tunasikitishwa sana na matukio haya ya
mauaji kijana mdogo amefariki dunia kwa sababu ambazo zingeweza
kuepukika kwa kutaka kumdhuru askari kwa kutumia silaha za jadi akiwa na
wenzake takriban 20 ili kukomboa ng’ombe waliokamatwa hifadhini,
tunawaomba mjiepushe na matukio ya namna hii fuateni sheria na taratibu
za nchi ili mfuge bila bughudha.” Amefafanua Prof. Gabriel

Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel
akiwaongoza viongozi wenzake katika ziara hiyo akiwemo Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima, Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju na Mkurugenzi wa Idara
ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wamefika pia katika Kijiji cha
Lualaje Kata ya Lualaje Wilayani Chunya na kuzungumza na baadhi ya
wafugaji kufuatia matukio ya wafugaji hao kuingiza ng’ombe katika
Hifadhi ya Ruaha.

Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima amewataka
wafugaji hao kufuata sheria na taratibu za nchi na kwamba jeshi la
polisi litazidi kutoa ushirikiano kwa wafugaji hao katika matukio
mbalimbali yakiwemo ya kuwabaini baadhi ya wafugaji ambao wamekuwa
wakiingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi pamoja na kujihusisha na
uhalifu.

Naye Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju amewataka wafugaji kuwa
watulivu na walitambue Tangazo la Serikali Na. 20 la Tarehe 14 mwezi
Machi mwaka 2008, ambalo liliongeza eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na
kupunguza eneo la malisho katika Wilaya za Chunya na Mbarali hali
iliyosabisha baadhi ya maeneo waliyokuwa wakiyamiliki kubadilishwa
matumizi na kuwa ya hifadhi, ambapo suala hilo tayari linafanyiwa kazi
kwa maelekezo ya Rais Magufuli na kuwataka kutoingiza mifugo yao katika
eneo la hifadhi hadi serikali itakapotangaza maamuzi mengine.

Kuhusu kuainishwa
kwa mipaka kati ya vijiji na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pamoja na Pori
la Akiba la Ruangwa, akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kutoka katika
wizara hiyo Dkt. Maurus Msuha amesema serikali kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii itahakikisha inatuma timu ya wataamu katika maeneo
hayo ili kuweka alama maeneo ambayo wananchi yanawatatiza kufahamu
mipaka ya vijiji na maeneo ya hifadhi ili kuondoa migogoro kati ya
maeneo ya wakulima na wafugaji na mipaka ya Hifadhi ya Ruaha na Pori la
Akiba la Ruangwa.

Baadhi ya
wananchi katika Wilaya za Chunya na Mbarali waliopata fursa ya
kuzungumza wakati wa ziara ya makatibu wakuu kutoka Wizara za Mifugo na
Uvuvi, Maliasili na Utalii, Mambo ya Ndani ya Nchi na Sheria na Katiba
wamesema wamefurahishwa na ziara hiyo na kwamba watazingatia maelekezo
waliyopatiwa ili kuhakikisha wanafuga kwa kufuata sheria na kwamba
watashirikiana na serikali ili kuwabaini baadhi ya wafugaji wanaokiuka
sheria na kuingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi ya Ruaha na Pori la

Wakizungumza kwa
nyakati tofauti wamefafanua kuwa wamefurahishwa kwa viongozi hao wa juu
kutoka wizarani kufika hadi katika maeneo yao na kujionea changamoto
mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya maji na malisho pamoja na kupata
taarifa za matukio ambayo yamejitokeza katika wilaya hizo kutoka mamlaka
mbalimbali za serikali wakiwemo viongozi wa serikali, wafugaji pamoja
jeshi la polisi.

Awali kabla ya
makatibu wakuu hao kutembelea wafugaji katika Wilaya za Chunya na
Mbarali, wamefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mbeya na kuwa na mazungumzo na
mkuu wa mkoa huo Mhe. Albert Chalamila pamoja Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Mbeya, ambapo Mhe. Chalamila amewaambia serikali ya
mkoa huo itaendelea kufanya kazi kwa kusimamia sheria na kuwaasa
viongozi wenzake wanapofika mkoani hapo kupata taarifa sahihi ya mkoa
kabla ya kufika katika maeneo mbalimbali kuzungumza na wananchi.

Aidha Mhe.
Chalamila amebainisha kuwa migogoro ya wafugaji katika Wilaya za Chunya
na Mbarali ambao wamekuwa wakiingiza mifugo kwenye maeneo ya Hifadhi ya
Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa katika Mkoa wa Mbeya unatokana na
wafugaji kuwa na mifugo mingi tofauti na maeneo ya malisho, hali ambayo
imekuwa ikiulazimu uongozi wa mkoa kutoa elimu kwa wafugaji juu ya
ufugaji wa kisasa na wenye tija kwa wafugaji kuwa na ng’ombe wachache
wanaoweza kuwapatia matokeo mazuri.

Ameongeza kuwa
uongozi wa Mkoa wa Mbeya utazidi kusimamia na kutoruhusu mifugo
kuingizwa katika maeneo ya hifadhi pamoja na maeneo yaliyotengwa kwa
ajili ya uhifadhi wa mazingira ili kuhakikisha mkoa huo unakuwa na
mpango wa matumizi bora ya ardhi.

ya makatibu wakuu wanne Mkoani Mbeya, ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara
ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akiambatana na
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima,
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju na
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha akimwakilisha
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda, ilikuwa na
lengo la kupata taarifa sahihi ya hali ya wafugaji katika Wilaya za
Chunya na Mbarali pamoja na kupata hadidu za rejea ambazo wataalam
watatumia katika kufanya mapitio na maboresho ya Tangazo la Serikali
(GN) Na. 28 la Mwaka 2008 ili iwe shirikishi na kupata suluhu ya
migogoro ya wakulima na wafugaji.