Sheikh afukuzwa kazi kwa kumuoa mwanaume mwenzake akidhani ni mwanamke

Imam aliyemuoa mwanamume mwenzake akidhani ni mwanamke amefutwa kazi na baraza kuu la Waislamu Uganda.
Huku mjadala kuhusu kama kweli alifahamu jinsia ya bi harusi wake wiki
mbili zilizopita alipofanya nikka naye, baraza hilo linasisitiza kuwa
kuna dosari kubwa kwa upande wa imam huyo na hastahili kuendelea na kazi
yake
Sheikh Mohammed Mutumba anadai kuwa alipata mshtuko wiki mbili baada ya
kugundua kuwa mke aliyemuoa aliyekuwa akivalia vazi la hijab kila wakati
na anafahamika kama Swabullah Nabukeera alikuwa ni mwanaume anayeitwa
Richard Tumushabe.
Ukweli kuhusu jinsia yake ulibainika baada ya polisi kumkamata Tumushabe
kwa madai ya wizi wa televisheni na nguo za jirani yake..
“Wakati polisi wakifanya shughuli zao za kila siku, askari wa kike
alimkagua sehemu zake za mwili kabla hajampeleka jela. Na kuwashangaza
maafisa wa polisi kuwa mtuhumiwa huyo kuwa aliweka nguo katika sidiria
ili aonekane ana matiti,”bwana Mugera alinukuliwa.
Sheikh Mutumba – ambaye ni imam wa msikiti uliopo kijiji cha Kyampisi ,
kilomita takribani 100 (62 miles) kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa
Uganda, Kampala – alidai kuwa hajafanya naye tendo la ndoa mke wake huyo
tangu amuoe kwa sababu alisema kuwa alikuwa ana matatizo ya kiafya
yaliyomfanya kuendelea kupata hedhi na ilimbidi amvumilie mpenzi wake.

Tayari tumemshtaki kwa kosa la kujiigiza kuwa mtu mwingine, vilevile kwa
kosa la wizi na kujipatia vitu kwa ulaghai ,” bwana Mugera alisema.
Gazeti la Daily Monitor limeripoti kuwa Sheikh Abdul Noor Kakande,
ambaye ni kadhi wa ukanda huo (jaji wa kiislamu), amesema kuwa tukio
hilo ni la kushangaza sana na halikubaliki, hivyo imam anafanyiwa
uchunguzi.
Vilevile Baraza kuu la Sheikh mkuu wa msikiti ambao sheikh Mutumba
anaswalia, Isa Busuulwa, amesema kuwa amemsimamisha kazi sheikh huyo kwa
heshima ya imani ya kiislamu hivyo hatoruhusiwa kuswalisha katika
msikiti wowote ule.
Baadhi ya wanawake nchini Uganda na wao wametowa hisia zao wakisema Imamu huyo kuna kitu anaficha:
“Haiingii akilini kwa namna moja au nyingine, hata kama ni mtu wa
kujifunika na tunaelewa waislamu wanajifunika sana.Lakini hawa watu
walifahamiana na kupelekana nyumbani ,na kwa muda wa wiki mbili kuna
mambo mengi kati ya mume na mke, kuna kuoga,kubadilisha nguo,
kuangaliana na mambo mengine mengi”
“Nataka kuuliza huyu imamu hajui utofauti wa mwanaume na mwanamke kwa
muda wote wa wiki mbili, ina maana hajawahi hata kumkumbatia?”
Msemaji wa polisi mkoa maalum wa polisi wa Ssezibwa Hellen Butoto
amefahamisha BBC kwa njia ya simu kuwa mtuhumiwa bado amehifadhiwa kituo
cha polisi Kayunga na amefunguliwa mashitaka
“Sasa mutuhumiwa anasubiri kufikishwa mahakamani kusomewa mashitaka ya kudaganya maumbile yake”.
Chanzo- BBC