Rais magufuli awaapisha mabalozi wanne

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo
amewaapisha Mabalozi Wateule wanne watakaoiwakilisha Tanzania katika
nchi za nje.

Walioapishwa ni;
1. Meja Jenerali (MST) Gaudence Milanzi kuwa Balozi wa Africa Kusini.

2.Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Balozi wa Namibia.

3.Prof. Emmanuel David Mwaluko Mbennah kuwa Balozi wa Zimbabwe.

4.Dkt. Benson Alfred Bana kuwa Balozi wa Nigeria.