KATIBU
Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu kulia akitoa cheti kwa
Maria Gaspar ambaye amenufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo
rasmi kwa mwaka 2019 wakati wa halfa ya utoaji wa vifaa venye thamani ya
Sh.milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la BRAC Tanzania kwa wasichana
ambao walinufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa
mwaka 2019 kulia ni Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo Manoah
William
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu kulia akitoa cheti
kwa Salma Hassani ambaye amenufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya
mfumo rasmi kwa mwaka 2019 wakati wa halfa ya utoaji wa vifaa venye
thamani ya Sh.milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la BRAC Tanzania kwa
wasichana ambao walinufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo
rasmi kwa mwaka 2019 kulia ni Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo
Manoah William
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu kulia akitoa vifaa
kwa Zawadi Salim ambaye amenufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya
mfumo rasmi kwa mwaka 2019 wakati wa halfa ya utoaji wa vifaa venye
thamani ya Sh.milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la BRAC Tanzania kwa
wasichana ambao walinufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo
rasmi kwa mwaka 2019 wa pili kutoka kushoto ni ni Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo
Manoah William na
KATIBU
Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu kulia akitoa vifaa kwa
Tatu Sajala ambaye amenufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya
mfumo rasmi kwa mwaka 2019 wakati wa halfa ya utoaji wa vifaa venye
thamani ya Sh.milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la BRAC Tanzania kwa
wasichana ambao walinufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo
rasmi kwa mwaka 2019 kulia ni Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo
Manoah William
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu akizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo
Manoah William akizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo
Manoah William akizungumza
Afisa Maendeleo ya Jamii kwa Jiji la Tanga Saimoni Nende
mmoja kati ya wanufaika kwenye mradi huo akizungumza
Sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa
Sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa
Sehemu ya wanufaika kupitia mradi huo wakifuatilia masuala mbalimbali
Tanzania limetoa msaada wa vifaa venye thamani ya Sh.milioni 29 kwa
wasichana ambao walinufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo
rasmi kwa mwaka 2019.
Akizungumza wakati wa halfa ya utoaji wa vifaa hivyo,
Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo Manoah William alisema
wasichana hao ni wale ambao hawakuweza kufanikiwa kufanya vizuri kwenye
mitihani yao katika mpango huo ambao walikuwa wakiutekeleza kwa
kushirikiana na serikali.
Alisema mpango huo ulianza mwezi Septemba mwaka huu kwa
kushirikiana na serikali kupitia Shirika la viwanda vidogo vidogo (Sido)
ambao mabinti zaidi ya 120 walipelekwa kwenye mafunzo na kujifunza
ujasiriamali na stadi mbalimbali.
Manoah alisema katika mafunzo hayo yalijifunza aina mbili
ya usindikaji wa chakula na kutengeneza sabuni ambao wanaamini itakuwa
mkombozi kwao kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao.
“Licha ya kutokufanikiwa lakini bado walitakiwa kuendelea
na elimu shirika likaona hapana kwa sababu hawakufanikiwa hai maanishi
kwamba watashindwa kuendelela kimaisha kwa hiyo tukawa na mpago wa
kuwasaidia na kuweza kupata mafunzo haya”Alisema
“Tunaamini mafunzo walioyapata wataweza kujiajiri wenyewe
tunawashukuru sido baada ya kupokea vyeti wanafunzi hao wataendea
kupata sapoti kwa sido moja kwa moja ikitokea washiriki maonyesho,
mashindano mbalimbali na Sido watakuwa sambamba nao”Alisema
Hata hivyo alisema pia mradi huo utafanikiwa zaidi ili
kuweza kuwaunganisha na Shirika la Viwango nchini (TBS) ili bidhaa zao
ziweze kutambulika na kuwa wafanyabishara wao wanajisikia fahari.
“licha ya watu kushindwa kuendelea na shule lakini
wamefanikiwa kujiajiri na kuajiri baada ya hapa mpango wetu ni kuendelea
kuwafuatilia kuona wanaendele na kazi zao kwa kushirikiana na serikali
za kata,mitaa na wilaya ili kuona wanaendeleaje”Alisema
Awali akizungumza katika halfa hiyo Katibu Tawala wa
wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim alisema alilishukuru Shirika la BRAC
Tanzania kwa kuisaidia serikali katika kuhakikisha wasichana walio nje
ya mfumo rasmi wanapata elimu ili kutimiza ndoto zao.
Alisema kwani wanapokuwa wakiwasaidia mabinti hao
wanakuwa wameisaidia jamii nzima hivyo niwapoingez sana kwa kusaidia
serikali kuongeza vipato vya wananchi.
“Wapo wasichana wengi sana mtaani lakini nyie leo
mmebahatika kufika hapa nawasihi mkatumie vema vifaa mlivyopewa kuweza
kujikwamua kiuchumi na sio vyenginevyo “Alisema
Aliwaasa pia kuhakikisha vifaa hivyo wanavitumia kwa
malengo yaliyokusudiwa ili viweze kuwa chachu yao kuweza kujikwamua
kiuchumi wao na jamii zinazowazunguka
“Lakini pia nawaasa mafunzo mliyopewa mkayafanyie kazi na
tafuteni wateja pia jitahaidini kutafuta masoko na kutengeneza ubora wa
bidhaa zenu ambazo mtakuwa mkizalisha”Alisema
Naye kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kwa Jiji la
Tanga Saimoni Nende alisema kwamba kazi iliyofanywa na Shirika la BRAC
Tanzania nzuri na inapaswa kupongezwa.
“Kwa kweli nimefurahishwa na Shirika la BRAC kazi kubwa
mnayofanya ya kuwaendesha wasichana walio nje ya mfumo rasmi wa masomo
najua wengi hawakupenda kukutana nah alai hii lakini mlipata tatizo
kutokana na mazingira yaliyokuwepo”Alisema
wasichana hao kwamba walichokipata wakakitumuia vizuri kiweze kuwasaidia
huku akieleza kwa waliopata ujuzi huo katika kata mbalimbali wao
wataendelea kuwafuatilia na kuwa karibu nao.