Shirika la compass lapanda na kugawa miche ya miti zaidi ya 400 kata ya tinde mkoani shinyanga

Katika taarifa yake mkurugenzi wa shirika
la Compass Rosemary Ndegeya amesema shirika hilo limegawa miche hiyo katika
shule ya sekondari ya wasichana Tinde, shule  ya Sekondari Kituli, kituo
cha afya Tinde, na Mamlaka ya Mizani kituo cha Tinde.

Mkurugenzi huyo amezihimiza taasisi hizo
kuitunza miti hiyo ili iweze kukua na kuleta matokeo chanya katiki jamii huku
akiiomba ofisi ya mazingira  kusimamia uendelevu wa utunzaji wa mazingira
ili kufikia malengo.

“Compass Tanzania ni shirika lisilokuwa la kiserikali
lililoanzishwa mwaka 2022 chini ya sheria ya NGO Namba 24 ya mwaka 2002. Kama
Jinsi tunavyojua kazi ya kifaa Compass yaani Dira, shirika letu lina ndoto ya
kuwa dira ya mafanikio kwa wananchi wote Tanzania tukianza na Mkoa wa
Shinyanga. Kauli Mbiu yetu ni… COMPASS TANZANI…. Njia ya mafanikio (the path to
success)”.

“Dira yetu ni kuona 
jamii iliyojengewa uwezo na yenye miradi ya kimaendeleo yenye matokeo
makubwa ili kuifika ndoto yetu, Compass Tanzania imejikita katika shughuli za
utunzaji wa mazingira, utetezi wa haki za binadamu na utekelezaji wa miradi
yenye matokeo makubwa huku tukipinga aina zote za unyanyasaji wa kijinsia”.
amesema Mkurugenzi Rosemary

“Malengo ya shirika hili ni kuhamasisha miradi ya ki
maendeleo yenye ushiriki wa wanaichi na ufanya utetezi na ulinzi wa haki za
binadamu hasa wanawake na Watoto Compass Tanzania inatekeleza shughuli zake
Tanzania bara, kwa namna ya Pekee Tumeanza na Mkoa wa shinyanga, Taaasisi yetu
ilitambulishwa Ngazi ya Mkoa na kupokelewa mapema mwaka huu 2023. Mara tu baada
ya kupokelewa na kupewa kibali cha kutekeleza shughuli zake, Taasisi yetu
kupitia meneja Miradi Mkoa wa Shinyanga ngudu Boniface Mhana tulianzisha kitalu
cha miti kupitia fedha zetu za ndani”.
amesema
Mkurugenzi Rosemary

“Leo tumekutana hapa baada ya kupokea maombi ya micha
ya miti ambapo Compass Tanzania imeandaa kitalu cha miti takribani 500 hapa
Tinde na Tabora manispaa, kitalu hiki kina thamani ya Tzs 2,500,000. Kwa maombi
tuliyopokea kwa awamu hii ya kwanza tunatarajia kugawa miti 400 yenye thamani
ya Tsh, 400,000. zoezi hili litaendelea mpaka kufikia malengo yaliyokusudiwa”.

“Miti tunayoigawa leo ni aina ya mitiki (white teek)
miti hii inatumika kuzalisha mbao nyeupe yenye thamani kubwa hapa Tanzania na
nje ya nchi mithili ya mti pendwa wa Mninga. Miti hii hustahimili ukame na
hutoa mazao makubwa baada ya miaka 8-10 inastahili kuvunywa, miti hii pia hutoa
kivuli na kuni kwa mahitaji ya nyumbani pia tuna mti wa mlonge ambao hutumika
kama dawa tiba mbadala na hutoa kuni na kuhifadhi mazingira kwa ujumla”.
amesema Mkurugenzi Rosemary

“Tunaomba Serikali itambue jitihada hizi za shirika
letu na kutuweka kwenye kanzi data yake ndani ya Mkoa wa Shinyanga na
kutushirikisha pale inapowekekana katika shughuli mbalimbali za ki maendeleo”.

“Tunakaribisha taasisi kubwa za kimaendeleo zinazotoa
zuzuku katika maeneo ya utunzaji wa mazingira na haki za binadamu kushirikiana
na Compass Tanzania ili kuendeleza kazi hii”.
amesema
Mkurugenzi Rosemary

Akizungumza meneja miradi wa shirika la
Composs Bwana Boniface Mhana amesema shirika hilo linatekeleza mradi  wa
kutunza  mazingira katika kata ya Tinde

Mgeni rasmi katika zoezi la upandaji na
ugawaji miche ya miti ni kaimu mkuu wa kitengo cha maliasili na uhifadhi wa
mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bwana Robet Anatory ambaye
amelipongeza shirika la Compass kwa kugawa miche ya miti huku akiwataka
wananchi wa kata ya Tinde kuunga mkono juhudi hizo.

Viongozi  mbalimbali waliohudhuria
zoezi hilo  wamelipongeza shirika la Compass kwa kugawa miche ya miti huku
wakiisihi jamii kuendelea kupanda miti ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na
serikakali.

Meneja miradi wa shirika la Compass Tanzania
Bwana Boniface Mhana akitoa elimu ya upandaji miti katika hafla ya kugawa miche
ya miti kwa wananchi, shule ya sekondari ya wasichana Tinde, shule  ya
Sekondari Kituli, kituo cha afya Tinde, pamoja na Mamlaka ya Mizani kituo cha
Tinde.