Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga
Mamla ya Majisafi na
usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) imetoa mapendekezo ya marekebisho ya Bei
za Maji kwa muda wa Miaka mitatu ikiwa
lengo ni kutatua changamoto zilizopo na kukidhi gharama za uzalishaji na
usambazaji wa Maji.
Akiwasilisha mapendekezo
hayo Mkurugenzi wa SHUWASA Mhendisi Yusuph Katopola amesema marekebisho hayo yatasaidia
kujiendesha kwa faida na kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Amefafanua kuwa bei hizo
zitaiwezesha mamlaka hiyo kuwa na uwezo mzuri wa kifedha ili kukidhi gharama za
uzalishaji na usambazaji wa Maji pamoja na gharama ya ununuzi wa Maji kutoka
KASHWASA.
Amesema SHUWASA imelenga
kuongeza mtandao wa maji na kuyafikia maeneo yote yenye uhitaji wa huduma hiyo
ambapo pia amebainisha bei zilizopendekezwa kwa makundi mbalimbali.
“Bei tulizopendekeza kwa kundi
la wateja wa majumbani ni shilingi 2550/= Mwaka (2023/2023), sh 3,190/= Mwaka (2024/2025)
na 3,630/= Mwaka (2025/2026) kutoka sh. 1740/= kwa sasa unit moja na huduma za kurejeshewa huduma ya
maji baada ya kusitishiwa kutoka sh. 10,000/= hadi sh. 15,000/= lakini ada za
maunganisho mapya ya huduma ya maji hii hatujapendekeza makundi yote
yataendelea kutoa asilimia 20 ya vifaa vya maunganisho”.amesema Mkurugenzi SHUWASA Mhandisi
Katobola
Mhandisi Katopola amezitaja
sababu za kuomba marekebisho ya bei za maji kuwa ni pamoja na kuisha kwa muda
wa bei za awali, kuongezeka kwa bei ya jumla ya kununua maji kutoka KASHWASA,
uwepo wa kodi na ushuru mbalimbali, kupanda kwa gharama za
uendeshaji kuongezeka kwa maeneo ya kutoa huduma.
Mkurugenzi huyo ameongeza
kuwa SHUWASA imelenga kusafirisha maji
safi na bora kwa wateja, kuendelea kusambaza mabomba hadi kwenye maeneo ya nje
ya mji, kujenga mitambo ya kuchakata majitaka ambapo amesema changamoto
zilizopo ni pamoja na mwamko mdogo wa wananchi kulipia bili ndani ya siku 30.
Wananchi walioshiriki
mkutano huo wamekuwa na maoni tofauti kuhusu mapendekezo hayo ambapo baadhi yao
wameonesha kuridhishwa na mapendekezo hayo huku baadhi wakionesha
kutoridhishwa.
Mwakilishi kutoka Baraza
la ushauri la serikali (GCC) Mr. Julius Mwambaso ametoa ushauri unaolenga
kumsaidia mtumiaji wa maji huku akiisisitiza mamlaka ya majisafi na usafi wa
mazingira Shinyanga SHUWASA kutekeleza kwa vitendo yale watakayokubaliana.
“Sisi
wataalam au Baraza ambalo linawataalam wote rimeridhishwa na ukokotoaji
msisitizo tu tunaweka ni kwamba ni kuhakikisha SHUWASA mnatekeleza kwa vitendo
haya mambo yote ambayo mmeyasema kuwa mtayafanya”.amesema
Mwambaso
Kwa upande wake
mwakilishi kutoka Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na Maji EWURA
CCC Bwana Joseph Ndatala ametoa ushauri wake.
“Kwa
kuwa bei za maji za SHUWASA kwa sasa ziko juu zitaumiza wateja hawa ambao wengi
wao ni wenye kipato cha chini hivyo Baraza la EWURA CCC linashauri bei hizo
zibaki hivyo hivyo kama zilivyo kwa sasa
lakini pia Baraza linashauri pawepo na ongezeko dogo tu ambalo halitakuwa na
madhara kwa watumiaji katika makundi haya”.amesema Ndatala
Awali mgani rasmi wakati akifungua mkutano
huo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph
Mkude amesema hatua hiyo itachochea ufanisi katika utoaji wa huduma kwa mamlaka
ya maji safi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA).
DC Mkude ametumia nafasi hiyo
kuwaomba watumiaji wa maji kutoa maoni yao kwa kujenga hoja bila upendeleo na
kuhakikisha wanashirikiana ili kuwa na makubaliano ya pamoja.
Meneja wa EWURA kanda ya ziwa George Mhina amesema mkutano huu ni sehemu ya
uchunguzi unaofanywa na EWURA kwa lengo la kupata maoni ya wadau wa huduma ya
majisafi na usafi wa mazingira kabla ya kutoa maamuzi kuhusu maombi
yaliyowasilishwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga SHUWASA
ambapo amesema utaratibu huo wa kukusanya maoni ni moja ya
njia za kutekeleza azma ya Serikali ya utawala bora kwa maana ya kuwashirikisha
wananchi katika kufanya maamuzi.
Mamlaka ya uthibiti wa
huduma za nishati na maji imefanya mkutano na wadau wake kwa lengo la kupokea
maoni kuhusu maombi ya marekebisho ya bei yaliyowasilishwa na SHUWASA ambapo
zoezi la kupokea maoni litaendelea kwa njia ya maandishi hadi Agosti 29 Mwaka
huu 2023.
Mkurugenzi wa mamlaka ya
majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhendisi Yusuph Katopola akiwasilisha
mapendekezo ya bei za maji kwa wadau leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM
Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa EWURA kanda ya ziwa George Mhina akizungumza kwenye taftishi
iliyolenga kupokea ombi la kurekebisha bei za maji kutoka mamlaka ya maji safi
na usafi wa mazingira Shinyanga leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa
mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu
Mhe. Joseph Mkunde awali akifungua mkutano huo uliolenga kupokea mapendekezo ya
bei mpya za maji leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa
Shinyanga.
Mwakilishi kutoka Baraza
la ushauri la serikali (GCC) Mr. Julius Mwambaso akitoa ushauri kwenye mkutano
huo leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.
Mwakilishi kutoka Baraza
la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na Maji EWURA CCC Bwana Joseph
Ndatala akitoa ushauri kwenye mkutano huo leo Jumanne Agosti 22,2023 katika
ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano ukiendelea leo
Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga
Zoezi la wananchi na wadau mbalimbali
kuwasilisha maoni yao juu ya bei za maji likiendelea katika ukumbi wa CCM Mkoa
wa Shinyanga.
Zoezi la wananchi na wadau mbalimbali kuwasilisha maoni yao juu ya bei za maji likiendelea katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mkurugenzi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhendisi Yusuph Katopola akijibu maswali yaliyoulizwa kwenye kikao hicho leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.