Skauti wilaya ya shinyanga waadhimisha nyerere day, madam veronica awasihi wananchi kuendeleza umoja na ushirikiano.


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Naibu kamishna wa Skauti katika Wilaya
ya Shinyanga Veronica Marwa amewasihi wakazi wa wilaya ya Shinyanga kumuenzi Baba
wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuendeleza hali ya umoja,
ushirikiano na amani.

Ameyasema hayo  Jumamosi Oktoba 14 wakati
vijana wa Skauti Wilaya ya Shinyanga wakiadhimisha kumbukizi ya miaka 24 ya
kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julias Nyerere, ambapo vijana hao
wameadhimisha kumbukizi hiyo kwa kufanya matembezi ya amani na shughuli
mbalimbali za kijamii ikiwemo usafi wa mazingira na upandaji wa miti.

Naibu Kamishina huyo amesema kupitia
matembezi hayo ya amani yamelenga kuhamasisha wananchi juu ya upandaji wa miti
pamoja na usafi wa mazingira huku akiwaomba wakazi wa Wilaya ya Shinyanga
kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua uchumi wa Taifa.

“Katika
kuhamasisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira tumepanda miti zaidi ya mia moja
lakini baadhi ya miche tumewagawia wananchi ili nao washiriki katika tukio la
leo, nawaomba tuendeleze umoja wetu na mshikamano lakini pia usawa wa kijinsia
tufanye kazi tuendelee kumuunga mkono Rais wetu wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa jitihada anazozifanya katika kukuza uchumi wa Nchi yetu lakini pia
uchumi wa mtu mmoja mmoja”.
amesema Madam Veronica

Kwa upande wake Afisa mazingira wa
Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga amesema ni muhimu kutunza mazingira
ili kuepukana na athari mbalimbali huku akiwasisitiza wakazi wa Manispaa ya
Shinyanga kuchukua tahadhari za uwepo wa mvua za El nino.

Mtendaji wa Kata ya Mjini Bwana Simon
Mashishanga kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga amewapongeza vijana wa
skauti kwa kuadhimisha siku hiyo.

Vijana wa Skauti Wilaya ya Shinyanga leo
Jumamosi Oktoba 14,2023 wamefanya matembezi ya amani yaliyolenga kuhamasisha
wananchi juu ya utunzaji wa mazingira ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 24
ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Skauti Wilaya ya Shinyanga wakiwa katika
matembezi ya amani ya kumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ambayo yamefanyika Jumamos Oktoba 14,2023 katika Manispaa ya
Shinyanga.

Skauti Wilaya ya Shinyanga wakiwa katika
matembezi ya amani ya kumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ambayo yamefanyika  Jumamos Oktoba 14,2023 katika maeneo mbalimbali
ya Manispaa ya Shinyanga.

Skauti Wilaya ya Shinyanga wakiwa katika
matembezi ya amani ya kumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ambayo yamefanyika  Jumamos Oktoba 14,2023 katika maeneo mbalimbali
ya Manispaa ya Shinyanga.