Smaujata mkoa wa shinyanga yatoa elimu ya ukatili kwa vijana wanaocheza mpira katika shirika la ajibika youth initiatives.


Na Mapuli Misalaba, ShinyangaKampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga leo Novemba 21,2023 imetoa elimu ya ukatili kwa vijana wanaocheza mpira wa miguu katika  shirika la AJIBIKA YOUTH INITIATIVES kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya pamoja na Mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Bi. Stella Gershom wamelipongeza shirika la hilo  kwa kuanzisha bonanza la michezo ambalo linawasaidia vijana hao kuepukana na vishawishi vya kuingia kwenye makundi mabaya ambapo badala ya kwenda kuzurula wanakutana kila siku kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu.Viongozi hao wa kampeni ya SMAUJATA wamewasisitiza vijana kuendelea kupenda michezo na kwamba hatua hiyo itawasaidia kuepukana na mambo yasiyofaa katika jamii ikiwemo kufanya matendo ya ukatili kama vile kulawiti , kubaka na wizi.Wamewaomba vijana hao kuwa mabalozi wazuri wa kupinga ukatili unaoendelea kufanyika kwenye jamii ikiwemo kutoa taarifa za watu wanaofanya ukatili kwenye maeneo yao ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa na serikali.Aidha wametaja sehemu za kutoa taarifa za ukatili ni ofisi za serikali za mitaa kwa wenyeviti, dawati la jinsia na watoto Polisi, kutoa taarifa kwa afisa ustawa wa jamii, afisa maendeleo ya jamii, kwa viongozi wa SMAUJATA au kupiga simu namba ya bure 116.Timu hizo ni Ajibika junior na timu ya Ajibika Fc ambapo mkurugenzi wa shirika la AJIBIKA YOUTH INITIATIVES Bwana Samwel Zebedayo Shaban amewashukuru viongozi  wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kuwatembelea na kutoa elimu ya ukatili ambapo amesema ataendelea kushirikiana na kampeni hiyo katika kupambana na ukatili wa kijisia unaofanyika kwenye jamii.Nao baadhi ya wachezaji wa tibu ya Ajibika junior kuanzia Miaka 10 hadi 18 na timu ya Ajibika Fc kuanzia Miaka 18 hadi 40 wameshukuru kwa kupata elimu sahihi ya ukatili ambapo wameahidi kupaza sauti  juu ya ukatili unaofanyika katika jamii ikiwemo kutoa taarifa za ukatili sehumu husika.SMAUJATA ni kampeni huru ya kupinga ukatili Nchini iliyoanzishwa na Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Shujaa Sospeter Bulugu kwa kushirikiana na Waziri wa wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
wakiendelea kutoa elimu ya ukatili kwa wachezaji wa tibu ya Ajibika junior na
timu ya Ajibika Fc kutoka shirika la shirika la AJIBIKA YOUTH INITIATIVES Manispaa
ya Shinyanga.