Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai akifuatilia mada mbali mbali kwenye Kongamano la viongozi wa dini lililoandaliwa na Bunge na Nacopha lililofanyika jijini Arusha kwenye ukumbi wa hotel ya Mount Meru
Ahmed Mahmoud, Arusha
Serikali imeeleza kuwa suala la elimu ya masuala ya vvu kwa jamii ni jambo endelevu na linatakiwa kuendelea kutolewa hususani kwenye suala la unyanyapaa ambalo limendelea kushika kasi kwa watu wanaoishi na maambukizi ya ukimwi.
Akiongea kwenye mkutano wa viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali ulioandaliwa na Bunge na Baraza la watu walioishi na VVU Spika wa bunge Job Ngugai alisema kuwa katika umoja wao viongozi wa dini wanauwezo wa kuvunja ukimya kuondoa ubaguzi na unyanyapaa.
Aliwaeleza kuwa walibebe suala hilo la unyanyapaa kwa kuwa umekuwa ubaguzi watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kwa kutoa elimu na kuhamasiha watu kuacha unyanyapaa kwenye jamii yetu.
“Tulikatae neno waathirika wa ukimwi tuwaite watu wanaoishi na maambukizi ya ukimwi ndani ya jamii ili kuondoa unyanyapaa unaopelekea ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU ili kuongeza jamii iishi na watu hao bila unyanyapaa” alisema Spika
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids Dkt.Leonard Maboko alisema kuwa elimu ndio suluhisho la unyanyapaa na kuondoa maambukizi mapya kwa watu kueleza kweli juu ya kupata maambukizi ili takwimu ziweze kusaidia Serikali.
Alisema asilimia 61 ya watu wanaoishi na maambukizi ya ukimwi walipoandika dodoso walisema hawana maambukizi jambo lililoonyesha kuwa ni sawa na asilimia 52 tulipopitia tukakuta ni aslimia 61 hivyo utoaji wa kweli wa taarifa utasaidia kuongeza utumiaji wa dawa za kufubaza na kufikia maambukizi sifuri ifikapo mwaka 2030.
Awali kaimu mufti Ally Ngeruko alisema kuwa suala la wanaoishi na maambukizi ya ukimwi kufanyiwa ubaguzi halikubaliki nalinatakiwa kupigwa vita kwenye jamii yetu hata uislamu unakataza hilo kwa kuwa Mungu anaweza kumrehemu na akakupa wewe.
Alisema anaishukuru Sana Serikali kwa kuitisha kikao hicho ambacho kinalenga kuondoa unyanyapaa kwenye jamii yetu hususani ndani ya Imani ambapo mtu mwenye virusi hivyo hawezi kutimiza nguzo ya tano ya uislam.
Nae Askofu mkuu wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania Dkt.Fredrick Shoo alisema kuwa anaamini viongozi wa dini wakihubiri na kutoa elimu juu ya kupiga vita unyanyapaa kwa watu wanaoishi na maambukizi ya ukimwi itasaidia kufikia malengo ya watanzania na jamii kutoendelea na unyanyapaa na hivyo taifa kufikia malengo ya kutokuwa na maambukizi mapya.
Alisema kuwa Serikali ikishirikiana na wadau na viongozi wa dini kufikia malengo ya utoaji elimu kukumbushana itasaidia kupunguza suala zima la ubaguzi kwa watu wanaoishi na maambukizi ya ukimwi hapa nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Baraza la waislamu nchini Bakwata Sheikh Khamis Mataka alisema kuwa ubaguzi ndani ya dini ya kiislamu haukubaliki hivyo suala la unyanyapaa nalo pia halikubaliki na kutoa wito kwa maimamu nchini kuwa mstari wa mbele kulipiga vita na kulisemea jambo hilo.