Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi [SACP] – ULRICH MATEI.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mbeya, Mrakibu Msaidizi wa Polisi [ASP] JANETH MASANGANO.
Jana Novemba 24, 2019 umefanyika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uchaguzi huo kwa Mkoa wa Mbeya umefanyika kwa amani na utulivu. Zoezi la kuhesabu kura limefanyika katika vituo vya kupigia kura na kwa sasa zoezi linaloendelea ni majumuisho ya kura na kutangaza matokeo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa nane [08] kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya kuvunja nyumba usiku na kuiba na kuwashambulia watu wengine.
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 00.20 usiku huko katika Kijiji cha Ndaga, Kata ya Ndanto, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
JUSTIN MANASI [27] na ELLY ARON MWASILE [27] mlinzi wote wakazi wa Nzunda walishambuliwa na kundi la watu wanaokadiliwa kufikia 10 waliokuwa wamevaa mizura.
Mbinu ni kuwashambuliwa kwa kutumia marungu sehemu mbalimbali za miili yao na kuwasababishia maumivu. Wahanga wamelazwa katika Hospitali ya Misheni Igogwe na
wanaendelea vizuri. Chanzo kinachunguzwa.
wanaendelea vizuri. Chanzo kinachunguzwa.
Aidha mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 01.00 usiku huko katika Kijiji cha Ndaga, Kata ya Ndanto, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
SABINA MUSA, [48] mkazi wa Ndaga alivunjiwa nyumba yake na kundi la watu wapatao 15. Mhanga alifanikiwa kuwatambua baadhi ya watuhumiwa kwa majina ambao ni:-
1. SADCK AMOS,
2. SHEDU MARTIN,
3. MOHAMMED YOHANA,
4. VICTOR JAPHET,
5. ELIUD SHAULI,
6. FURAHA YUNGI na
1. SADCK AMOS,
2. SHEDU MARTIN,
3. MOHAMMED YOHANA,
4. VICTOR JAPHET,
5. ELIUD SHAULI,
6. FURAHA YUNGI na
7. BENJAMIN BRAISON. Baada ya hapo watuhumiwa hao walivunja nyumba mali ya GEORGE EDWARD MWANAMTWA [61] mkazi wa Ndaga kisha kuiba kuku 2 wenye thamani ya Tshs 50,000/=.
Kufuatia matukio hayo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako tarehe 25.11.2019 majira ya saa 03:00 usiku huko kijiji cha Ndaga kilichopo Kata ya Ndanto, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kuwakamata
watuhumiwa nane [08] ambao ni:-
1. DANIEL PHILIPO [46]
2. JOSEPH MWANILEA MWAMPAMBA [50]
3. YOHANA CHETI MAHENGE [27] mwanafunzi MUST
4. MUSA PIMBA NGABO [40]
5. PWEKE AMOS [28]
6. JAPHET NJOBO [50]
7. DANIEL SWED [37]
8. BENJA VAKOPEGE NGAILO [30] wote wakazi wa Nzunda – Ndanto.
watuhumiwa nane [08] ambao ni:-
1. DANIEL PHILIPO [46]
2. JOSEPH MWANILEA MWAMPAMBA [50]
3. YOHANA CHETI MAHENGE [27] mwanafunzi MUST
4. MUSA PIMBA NGABO [40]
5. PWEKE AMOS [28]
6. JAPHET NJOBO [50]
7. DANIEL SWED [37]
8. BENJA VAKOPEGE NGAILO [30] wote wakazi wa Nzunda – Ndanto.
Msako mkali wa kuwakamata watuhumiwa wengine unaendelea. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika watafikishwa Mahakamani.
KUPATIKANA NA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA.
Mnamo tarehe 20.11.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko eneo la Mafiati, Kata ya Maanga, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata DEOGRATIUS JULIUS [27] Mkazi wa Soweto Jijini Mbeya akiwa na dawa zidhaniwazo kuwa za kulevya aina ya “Heroine” kete 27 akiwa amezificha kwenye mfuko wa suruali aliyovaa.
Baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alidai kuwa dawa hizo amepewa na mtu mmoja anayefahamika kwa jina la KELVIN DAVID MWANKUGA [28] Mkazi wa Mafiati Jijini Mbeya.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilianza msako mkali na mnamo tarehe 25.11.2019 majira ya saa 05:00 alfajiri huko maeneo ya Mwambene, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya mtuhumiwa KELVIN DAVID MWANKUGA [28] alikamatwa. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani.
UZINDUZI WA SIKU KUMI NA SITA [16] ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.
Aidha leo tarehe 25.11.2019 ni uzinduzi wa siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia. Lengo la siku 16 za kupinga ukatili ni kutoa mwanga wa uelewa kwa jamii kwa siku nyingine kama vile Novemba 29 ambayo ni siku ya kimataifa ya watetezi wa haki za wanawake.
Lakini pia Desemba mosi ni siku ya UKIMWI duniani, pia Desemba 06 ni siku ya kukumbukwa mauaji ya Montreal 1989 ambapo wanawake 14 waliuawa kikatili na mtu aliyekuwa anawachukia wanawake, wakati huo Desemba 10 ni siku ya haki za binadamu duniani ambapo hutoa fursa kwa wanawake na wanaume.
Jeshi la Polisi limekuwa likishiriki maadhimisho haya ya kimataifa katika kuhakikisha tunatoa elimu maeneo mbalimbali hususani katika mikutano ya hadhara, midahalo, makanisani na misikitini pamoja na kwenye vyombo vya usafiri, vyombo vya habari kwa
lengo la kuelimisha wananchi kuhusu masuala mazima ya ukatili na madhara yatokanayo na ukatili.
lengo la kuelimisha wananchi kuhusu masuala mazima ya ukatili na madhara yatokanayo na ukatili.
Kauli mbiu ya siku 16 za kupinga ukatili mwaka huu 2019 inasema “KIZAZI CHENYE USAWA SIMAMA DHIDI YA UBAKAJI”