Taifa star ‘baba lao’ full mzuka, yaichapa equitorial guinea 2-1

Na Mwandishi Wetu, APC BLOG DSM


TAIFA STAR ‘BABA LAO’ ndio tunavyoweza kusema kwa sasa baada ya kuibuka kidedea dhidi ya nchi ya Equitorial Guinea kwa kuichapa goli 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa Jijini hapa.

Stars
iliyo chini ya Etienne Ndayiragije iliyoanza kwa kasi kipindi cha
kwanza ikijiwinda vyema na michuano ya AFCON,  haikuweza kutumia vema nafasi saba za kipindi cha kwanza na
kuruhusu wapinzani wao Equatorial Guinea kuandika bao la kwanza dakika
ya 15 kupitia kwa Pedro Obiang akimtungua kipa mkongwe wa Tanzania, Juma
Kaseja kwa shuti la mbali.




Dakika
tano baada ya kuanza kipindi cha pili, kocha Mrundi wa Tanzania,
Etienne Ndayiragijje alianza na mabadiliko ya kuongeza nguvu katika safu
ys ushambuliaji, akimtoa beki wa kulia Hassan Ramadhani Kessy na
kumuingiza mshambuliaji, Ditram Nchimbi.

 


Ni
mabadiliko hayo yaliyoisaidia Taifa Stars kupata bao la kusawazisha
likifungwa na kiungo mshambuliaji wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco,
Simon Happygod Msuva dakika ya 68 akimalizia mpira uliookolewa na kipa
baaada ya yeye mwenyewe kuunganisha kwa kichwa kona ya beki wa kushoto,
Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

 


Taifa
Stars iliongeza kasi ya mashambulizi baada ya bao hilo na juhudi zao
zilizaa matunda dakika ya 90  baada ya kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar
Junior ‘Sure Boy’ kufunga bao la ushindi kwa shuti la mbali.

 


Baada
ya ushindi huo, Taifa Stars itasafiri kuwafuata Libya Uwanja wa
Mustapha Ben Jannet mjini Monastir Jumanne ya Novemba 19 kwa mchezo wa
pili wa kundi hilo.