Takukuru yamkamata mweka hazina wa kikundi aliyedai pesa zimeyeyuka kishirikina

Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha inamshikilia
Muweka hazina wa kikundi cha ujasiriamali cha Imani kwa tuhuma za
kutafuna Tsh.Million 39 za Wanakikundi na kudai zimeyeyuka kishirikina.


Wanakikundi 28 juzi walikesha wakilia nyumbami kwa Muweka hazina huyo
Halima Mwidadi Mkazi wa Osunyai Arusha baada ya kuambiwa fedha hizo
ambazo walitakiwa kugawana zimepotea katika mazingira ya kutatanisha.
Wengine waliokamatwa na TAKUKURU ni Katibu wa Kikundi Deogratius Seif na
Mwenyekiti wake Aisha Saidi ambao walikamatwa jana na kuachiwa kwa
dhamana huku Muweka hazina akiendelea kusota Mahabusu kwa sababu za
kiupelelezi