Zoezi la Uchukuaji fomu, Urudishaji fomu, Uteuzi, Pingamizi na Rufaa lilianza tarehe 29/10/2019 na kumalizika tarehe 9/11/2019.
zoezi hilo jumla ya wananchi 555,036 kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa
walifanikiwa kuchukua fomu za kugombea. Na jumla ya wananchi 539,993
sawa na asilimia 97.3 walifanikiwa kurejesha fomu.
kutoka Chama cha Mapinduzi waliochukua fomu walikuwa 412,872 (asilimia
74), Chama cha Demokrasia na Maendeleo walikuwa 105,937 (asilimia 19),
Chama cha Wananchi CUF walikuwa 24,592 (asilimia 4), ACT Wazalendo
walikuwa 8,526 (asilimia 1.5), NCCR – Mageuzi walikuwa 2,244 (asilimia
0.4) na Vyama vingine vyenye usajili
zoezi zima la kuchukua na kurejesha fomu kulikuwa na changamoto kubwa
kwa wagombea wengi kufanya makosa mengi ya kikanuni yaliyopelekea wengi
wao kutoteuliwa.
Baadhi
ya makosa hayo ni pamoja na kujidhamini wenyewe, kutojaza fomu namba
IV, kutofautiana kwa majina, kutojaza fomu kwa ukamilifu, kuandika umri,
kukosea umri (mfano amezaliwa mwaka 2019) na makosa mengine mengi
mbalimbali. Hii ilitokana na baadhi ya vyama kushindwa kuwajibika
ipasavyo katika kuwaelekeza wanachama wao. Kutokana na hali hiyo
pingamizi na rufaa mbalimbali zipatazo 15,380 ziliwasilishwa.
zoezi la maamuzi ya rufaa mbalimbali lilipohitimishwa tarehe 9/11/2019,
jumla ya rufaa 4,921 (32%) zilipitishwa na zilizobaki zilikosa sifa kwa
sababu mbalimbali.
mchakato huo wa kuchukua na kurudisha fomu Chama cha Mapinduzi
kimefanikiwa kupita bila kupingwa katika maeneo mbalimbali kwakuwa
hapakuwa na mgombea yoyote kutoka Chama cha Upinzani. Kwa upande wa
Wenyeviti wa Vijiji Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika
vijiji 6,248 kati ya vijiji 12,319 sawa na asilimia 51.
upande wa Mitaa Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika Mitaa
1,169 kati ya Mitaa 4,263 sawa na asilimia 27 Kwa upande wa Vitongoji
Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika Vitongoji 37,505 kati
ya Vitongoji 64,384 sawa na asilimia 58. Kwa upande wa Wajumbe wa kundi
la wanawake jumla ya wajumbe 64,085 wamepita bila kupingwa na wajumbe
kundi mchanganyiko jumla ya wajumbe 75,560 wamepita bila kupingwa.
kuwa imeonekana wazi wananchi kutoka vyama mbalimbali wamekuwa na nia
kubwa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi licha ya vyama vyao
kutokuweka umuhimu katika kuwaelekeza vyema wanachama wao juu ya ujazaji
fomu kwa mujibu wa Kanuni.
ya Uchaguzi imeona ni vyema wananchi hao kupewa nafasi ya kushiriki
katika Uchaguzi kwani imejidhihirisha wazi hata baada ya vyama viwili
vilivyojitoa bado wanachama wao waliendelea kuwasilisha rufaa zao ili
wapewe nafasi ya kushiriki katika uchaguzi.
mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2019 Tangazo la
Serikali Na. 371 la Mwaka 2019 Kanuni ya 49, Tangazo la Serikali Na.
372 la Mwaka 2019 Kanuni ya 51, Tangazo la Serikali Na. 373 la Mwaka
2019 Kanuni ya 52, na Tangazo la Serikali Na. 374 la Mwaka 2019 Kanuni
ya 52 ninatoa muongozo kwamba Wagombea wote ambao walioteuliwa na
kudhaminiwa na vyama vyao na kufanikiwa kurejesha fomu zao za uteuzi kwa
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika kipindi kilichokuwa kimepangwa
cha kuchukua na kurejesha fomu kilichoanza tarehe 29*/10/2019 na
kumalizika tarehe 04/11/2019 kwa Tangazo hili wanapewa sifa ya kupigiwa
kura na wananchi wa Kijiji, Mtaa, au Kitongoji husika kwa ajili ya
Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019 isipokuwa tu kama
atakuwa amekutwa na mambo yafuatayo:
Wamerejesha fomu watu zaidi ya mmoja kutoka chama kimoja kwa nafasi
inayofanana ya Mwenyekiti wa Kijiji, Mtaa, au Kitongoji kwa Kijiji,
Mtaa, au Kitongoji husika. Msimamizi Msaidizi hata wajumuisha wagombea
hao katika orodha ya wanaopaswa kupigiwa kura,
Amejitoa kwa mujibu wa Kanuzi za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tangazo
la Serikali Na. 371 la Mwaka 2019 Kanuni ya 19, Tangazo la Serikali Na.
372 la Mwaka 2019 Kanuni ya 20, Tangazo la Serikali Na. 373 la Mwaka
2019 Kanuni ya 20, na Tangazo la Serikali Na. 374 la Mwaka 2019 Kanuni
ya 20.
wa Uchaguzi ataanza kupokea ratiba za kampeni kutoka katika Vyama vya
Siasa kuanzia leo hii tarehe 10/11/2019 hadi kesho jioni kwa ajili ya
kuziunganisha.
ya matukio na shughuli zingine zote zinazohusu Uchaguzi huu zitaendelea
kwa mujibu wa Kanuzi za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019.