Tasaf yaleta matokeo chanya njombe



Na Mwandishi Wetu, APC BLOG, NJOMBE 
 


Mpango wa kunusuru kaya masikini nchini Tanzania TASAF
unaofadhiliwa na shirika la kimataifa la mafuta OPEC umetajwa kubadili
maisha ya wanufaika wengi katika Halmashauri ya mji wa Makambako Mkoani Njombe.
Imeelezwa kuwa hapo
awali wananchi wengi wa Makambako walikuwa wakiishi maisha duni lakini baada ya kupatiwa msaada huo hivi sasa wameenda katika kipato cha kawaida na wanaishi maisha mazuri kupitia msaada wa fedha kuendesha miradi ya kilimo, ufugaji n.k


Baadhi ya wanufaika ambao wameweka bayana mafanikio waliopata
na kukiri kubadilika kimaisha Ni pamoja na Amon Kidenya na Salome Mligo
ambao walipewa fedha na kuanzisha mradi wa ufugaji wa ng’ombe na kuku
na kufanikisha ujenzi wa nyumba ya kuishi huku mwingine akidai amekuwa
na uhakkika wa kupata milo zaidi ya mitatu.


Akifafanua namna mpango wa TASAF ulivyofanikiwa kutekeleza
miradi 48 yenye thamani ya bil 1.9 katika awamu ya kwanza inayotekelezwa
katika kipindi cha miaka 5 kwa kushirikiana na wananchi wanaochangia
asilimia 10 katika utekelezaji wa baadhi ya miradi mkurugenzi wa
halmashauri ya mji wa Makambako Paul Malala amesema ujio wa mpango huo
umekuwa na matokeo makubwa chanya kwa wananchi na serikali.


Malala amesema TASAF imefanikiwa kujenga vituo vya afya 3
,barabara 7 ,mabweni 5 ,madarasa 6 ofisi za walimu 2 na miradi mingine
ya ufugaji na kilimo Cha parachichi na mbao.


Wanafunzi nao akiwemo Amosy Makinge na Sabrina Sanga
 wanaeleza jinsi mpango huo ulivyosaidia kuboresha miundombinu ya elimu
kwa kujenga mabweni,darasa na vyoo na kurahisisha upatikanaji wa elimu
bora.


Lakini mafanikio yamekujaje kwa wanufaika mjini Makambako
ambao waliingizwa kwenye mpango wakiwa hawana uhakika wa mlo hata mmoja
na kusomesha watoto na kufanikiwa kupiga hatua kubwa kiuchumi na
kulazimika kupisha wengine wenye hali mbaya. Hapa mratibu wa TASAF
Makambako Veronica Simwanza anaeleza jitihada zilizochukuliwa.