Kaimu
Mkurugenzi Mkuu TBS Bw.David Ndibalema akifungua mafunzo yanayohusu
viwango na matakwa ya viwango vya mabati na koili yaliyofanyika leo
katika makao makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es
Salaam.
mafunzo
yanayohusu viwango na matakwa ya viwango vya mabati na koili
yaliyofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Viwango Tanzania
(TBS) Jijini Dar es Salaam.
Wazalishaji,wauzaji,wasambazaji
wa mabati na wadau mbalimbali wakifuatilia mafunzo yanayohusu viwango
na matakwa ya viwango vya mabati na koili yaliyofanyika leo katika makao
makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Shirika
la Viwango Tanzania TBS limetoa mafunzo kwa
wazalishaji,waagizaji,wasambazaji na wadau mbalimbali wa mabati na koili
za mabati hapa nchini baada ya Tanzania kukamilisha utaratibu wa
kupitisha viwango vya mabati na koili ambavyo ni TZS 353:2020/EAS
11:2019 na TZS 1477:2020/EAS 468:2019 kuwa viwango vya kitaifa pamoja na
kiwango Na.1476:2017.
Akizungumza
wakati anafungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu TBS Bw.David
Ndibalema amesema shirika hilo lilifanya tathimini ambapo ilibaini kuwa
yapo mabati na koili za mabati zinazozalishwa na kuaingizwa hapa nchini
hazikidhi matakwa ya viwango.
“Mafunzo
haya yanalenga kuandaa washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa
liuweledi katika kuzalisha,kuingiza na kusambaza mabati na koili za
mabati zinazokidhi matakwa ya viwango”. Amesema Bw.Ndibalema.
Aidha
Bw.Ndibalema amesema TBS itaendelea kutilia mkazo kusimamia maswala ya
viwango na udhibiti ubora na kwamba biashara zinafanywa katika mifumo
inayoeleweka na kukubalika kisheria sambamba na kanuni zinazosimamia
mifumo viwango na udhibiti ubora.