Tcra yatoa elimu kwa wadau wa mawasiliano kanda ya ziwa yahimiza kutumia tanzanite portal kwa huduma za leseni.

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Mhandisi wa  Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA  idara ya leseni na ufuatiliaji kitengo cha
huduma kwa wateja Kadaya Baluhye amewaasa wadau wa mawasiliano ambao
wanahudumiwa na mamlaka hiyo  kutumia
mfumo wa Tanzanite Portal katika huduma za leseni.

Mhandisi Baluhye Ametoa
wito huo Machi 31,2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi
wa mikutano uliopo katika Hoteli ya Empire mjini Shinyanga wakati akitoa semina
ya jinsi ya kutumia mfumo huo.

Mhandisi Baluhye amesema
ni muhimu wadau wa mawasiliano ambao wanahudumiwa na TCRA kutumia mfumo huo
katika huduma za kuomba leseni pamoja na kuhuhisha leseni zao.

Mhandisi Baluhye ametumia
fursa  hiyo kuwataka wadau wa mawasiliano
ambao wanahudumiwa na TCRA kufuata sheria na taratibu zilizopo katika uwekaji
wa maudhui mtandaoni.

Mamlaka ya mawasiliano
Tanzania TCRA leo imefanya semina fupi ya utoaji elimu kwa wadau wake jinsi ya
utumiaji wa mfumo wa Tanzanite Portal kujisajili,kuomba na kuhuhisha leseni za
mawasiliano.