Tushirikiane kupigia mbiu lugha ya kiswahili :prof.mwamfupe

Mgeni
Rasmi katika akikata utepe katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja
la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua
Samwel Madumulla
Meya
wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe akimkabidhi kitabu Profesa
Joshua Samwel Madumulla kilichoandaliwa kwa heshima yake katika chuo
kikuu cha Dodoma kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kukuza,kuenzi
na kuendeleza lugha ya kiswahili katika chuo kikuu ca dodoma ,tanzania
na hata nchi jirani.
Meya
wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe akimpongeza  Profesa Joshua
Samwel Madumulla kwa kazi kubwa aliyoifanya hadi kuandaliwa kitabu kwa
heshima yake katika chuo kikuu cha Dodoma kwa kutambua mchango wake
mkubwa katika kukuza,kuenzi lugha ya kiswahili.
Profesa
Albino Tenge wa Rasi ya Ndaki ya Insia na Sayansi ya jamii Chuo Kikuu
cha Dodoma akitoa neno katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la
Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel
Madumulla
Pofesa Joshua Samwel Madumulla akiwa anazungumza na wageni waalikwa katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima yake iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Muwakilishi
wa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma Profesa Mwegoha akitoa neno katika
Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia
kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla

Mmoja
wa wanafunzi wa Profesa Joshua Madumulla Dkt.Abdulimalick Feruz
akichangamsha ubongo wa wageni waliohudhuria Hafla ya uzinduzi wa kitabu
cha Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa
Joshua Samwel Madumulla
Muwakilishi
kutoka Chama cha kusanifu Ushairi Tanzania Bi.Asia Kulastara akisoma
shairi katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia
kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanataaluma waChuo Kikuu cha Dodoma Dkt.Julius Ntwenya akitoa neno katika hafla hiyo
Wa
kwanza kushoto ni Profesa Hermans Mwansoko akiwa pamoja na Profesa
Joshua Samwel Madumulla,katika ukumbi wa Ukumbi wa Mihadhara Chuo Kikuu
cha Dodoma.

Wa
kwanza kushoto ni Profesa Hermans Mwansoko akiwa pamoja na Profesa
Joshua Samwel Madumulla Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis
Mwamfupe (anayeandika),wa kwanza kulia ni Dr.Athuman Ponera
Wa
kwanza kulia Mgeni Rasmi Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis
Mwamfupe (anayeandika) (katikati)Profesa Joshua Samwel Madumulla pamoja
na  Profesa Hermans Mwansoko
Wa
kwanza kulia Mgeni Rasmi Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis
Mwamfupe (anayeandika) (katikati)Profesa Joshua Samwel Madumulla pamoja
na  Profesa Hermans Mwansoko
Muasisi wa wazo kla kuandika kitabu cha Koja Koja
la Taaluma za Insia ambaye pia ni Mhariri wa kitabu hicho Dkt.Athuman
Ponera ,ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika chuo kikuu cha
kumbukumbu ya Mwal.Nyerere Kampasi ya Zanzibar,akiwa na Mhadiri wa Idara
ya Kiswahili Chuo kikuu cha Dodoma Dkt.Zuhura Badru ambaye naye alikuwa
mhariri mwenza wa kitabu hicho cha Koja walkiwa katika picha ya pamoja
na Profesa Madumulla.
Profesa Joshua Samwel Madumulla akikabidhiwa zawadi na mhadhiri msaidizi taaluma za kiswahili chuo kikuu ca Dodoma
Profesa Joshua Samwel Madumulla akikabidhiwa zawadi na mhadhiri msaidizi taaluma za kiswahili chuo kikuu  Dodoma
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Udom akimkabidhi Profesa Madumulla zawadi.
Profesa
Joshua Samwel Madumulla akipeana mikono na Dkt.Zuhura Badru mara baada
ya kumkabidhiwa zawa iliyoandaliwa na Idara ya Kiswahili chuo kikuu cha
Dodoma .
Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis akikionyesha kitabu mara baada ya kukata utepe.
Makabidhiano ya fedha mara baada ya mauzo ambapo ziliuzwa zaidi ya nakala 70 
Baadhi
ya washiriki waliojitokeza kuhudhuria Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha
Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua
Samwel Madumulla
Picha
ya pamoja ya baadhi ya washiriki katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha
Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua
Samwel Madumulla
Picha
ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi katika Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha
Koja la Taaluma za Insia kilichochapishwa kwa heshima ya Profesa Joshua
Samwel Madumulla

Na,Vero Ignatus,Dodoma.
Uzinduzi wa kitabu cha Koja la Taaluma za Insia  kilichotolewa
kwa heshima ya Profesa Joshua Samwel Madumulla umefanyika  Jijini
Dodoma katika Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ukiwa na lengo la kuenzi kazi
za wataalam wa lugha ya kiswahili na kutambua mchango wao katika kukuza
lugha hiyo
Akizungumza
katika uzinduzi huo mgeni rasmi ambaye ni Meya wa Jiji la Dodoma
Profesa Davis Mwamfupe amesema kuwa Lugha ya Kiswahili inazidi kutanuka
na kwenda mipaka nchi nyingine hivyo inafungua fursa za kibiashara baina
ya hizo
Profesa
Mwamfupe amesema kuwa Tanzania haiwezi kuwa na viwanda vya kuzalisha
kila kitu hapa nchini bali uchumi huo utakuwa umetekelezeka pale ambapo
kutakuwa na ushirikiano wa kibiashara kutoka kwa mataifa mengine ambapo
watu watanunua bidhaa hapa nchini hivyo lazima katikati ya mnunuzi na
mnunuaji kunakuwepo na umuhimu wa matumizi ya lugha.
Muwakilishi
wa makamu mkuu wa chuo cha Dodoma Profesa Mwegoha  amesema heshima ya
mwanataluma Pro.Joshua Mdumulla aliyopewa katika lugha ya Kiswahili
itachagiza watu wengi kukipenda Kiswahili na hivyo kusambaa katika
sehemu nyingi ndani ya nchi na nje ya nchi huku akitaka kuendelea
kuwaenzi wanataaluma waliotumia muda wao mwingi kuitumikia jamiii
kukumbukwa na kuthaminiwa sana hata watakapomaliza muda wao wa kitaaluma.
Akishukuru
mara baada ya kutunukiwa andiko la kitabu cha Koja la taaluma za Insha
Pro.Joshua Mdumulla alisema kuwa hapo awali walikuwa wamelala kuhusu
lugha ya Kiswahili kwani waliwaachia nchi jirani wakifanya mengi
kuonyesha kwamba wao ndiyo wenye Kiswahili,amesema Tanzania kwa sasa
imejikita katika kuhamasisha lugha ya Kiswahili huku wakiunga mkono
juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli za
kukuza kiswahili 
Amesema
kuwa anao uhakika kwamba kwa muda mfupi nchi ya Tanzania itapiga hatua
kubwa sana katika kukuza na kuieneza lugha hiyo,hivyo amewahimiza
watanzania kwamba washirikiane katika kukipigia mbiu lugha ya kiswahili
ili kiweze kuendelea na kuenea katika dunia
Akitoa
salamu kwa niaba ya wawakilishi waliowahi kuwa wanafunzi wa
mtambarukiwa  Prof.Madumulla ,Dkt Sanga:amesema kuwa amekuwa  ni mwalimu
wa pekee na heshma anayotunukiwa  amestahili,kutokana na mchango wake
katika lugha ya Kiswahili ambapo kwenye chou cha Dodoma idara ya
Kiswahili ina madaktari wengi ambapo yeye kasimamia elimu zao na siyo
kwa Dodoma tu bali Tanzania nzima.
Kwa
upande wake muwakilishi kutoka Jumuiya ya wataalamu UDOM kiongozi wa
Mwenyekiti wa UDOMASA Dkt.Julius Mtwenya amesema kuwa anamfananisha
profesa na mama wa kitanzania ambaye anaishi maeneo yasiyokuwa na
mtandao lakini bado aliendelea kuwalea Watoto katika mazingira magumu
lakini aliendelea kukesha na wanafunzi bila kujali.
Katika
hatua nyingine Dkt. Mtwenya amesema kuwa anamfananisha Prof. Mdumulla
na viongozi wa dini ambao wanatengeneza wafuasi wengi kwasababu kila
anapokutana na wanafunzi wenye shida aliweza kutatua hivyo imemfanya
 kumuona ni Tajiri mkubwa mwenye watu wengi

Tutaendelea
kuyaenzi na kuyaishi yale yote aliyoyaacha   kwani wanataaluma kutoka
Chuo kikuu cha Dodoma tunenufaika sana sana na elimu yake”alisema
 
Naye
Mkuu wa Idara ya Kiswahili Chuo kikuu cha Dodoma Dkt.Zuhura Badru
alisema kuwa Kiswahili ni lugha inayotumika katika nchi mbalimbali
katika nchi za Afrika,na nchini Tanzania lugha ya kiswahili inatumika
katika mawasiliano katika idara mbalimbali za serikali ikiwamo
Mahakamani,Bungeni na sehemu nyingine.
Dkt.Zuhura
alisema  kuwa idara ya Kiswahili itaendelea kuunga mkono juhudi za
serikali katika kukuza na kukienzi Kiswahili hapa nvhini na duniani
pote. 
Akitoa
salamu kutoka ofisi ya Rasi wa Ndaki ya Insia na Sayansi za jamii ya
Chuo kikuu cha Dodoma Prof.Albino Tenge wamempongeza Prof.Joshua Samwel
Mdumulla kwa mchango mkubwa kwa kuendeleza na kukuza Kiswahili na
kueleza kuwa ni mmoja wa waanzilishi wa chuo kikuu cha Dodoma na kusema
kuwa anao utajiri wa watu wengi walipitia miknoni mwake.
Ametoa
rai kwa wanafunzi waliokuwepo katika eneo husika watumie taaluma zao
kwa kuacha alama katika jamii zao na kukienzi Kiswahili ili jamii iweze
kutambua umhimu wa lugha hiyo.
Kwa
upande wake muasisi wa wazo la kuandika koja Koja la taaluma za Insha
Dkt.Ahuman Ponera amesema kuwa amesema Prof.Madumulla ni mwanataaluma
adhimu katika uga wa fasihi amekuwa mstari wa mbele katika kukuza na
kuendeleza lugha ya Kiswahili na fasihi kwa ujumla.

Dkt.Ponera
alisema kuwa amwekuwa miongoni   miongoni mwa wataalamu ambao wamekuwa
na mchango mkubwa kupitia utafiti na machapisho mbalimbali katika Nyanja
nyingi kama  vile riwaya ya Kiswahili,fasihi ya
Watoto,uandishi,uchapishaji,usomaji,uhakiki,fasihi simulizi na ujumi
Dkt.
Ponera amesema kuwa mbali na hayo Prof.Madumulla amewahi kushika
nyadhifa kwenye asasi mbalimbali baadhi ni amewahi kuwa mwenyekiti wa
kwanza wa ukuzaji wa vitabu Tanzania (1998-2002)mwenyekiti wa kamati ya
vitabu vya Watoto(1995-1999)mwenyekiti wa chama cha wasomaji Tanzania
(2000 hadi sasa)Amid mshiriki,(taaluma)kituo cha Sanaa na sayansi za
jamii (2000-2003)mjumbe kamati ya utafiti na uchapishaji ya utafiti na
elimu ya demokrasia Tanzania reserch and education for democracy in
Tanzania (REDET)ambapo alihariri machapisho kadha.
Adha
amesema nyadhifa nyingine ni pamoja mkuu wa idara ya Kiswahili chou
kikuu cha Dar es salaam(2004-2006)Amid skuli ya Sanaa na lugha chou
kikuu cha Dodoma (2007-2012)naibu Makamu mkuu wa chuo cha taaluma chuo
kikuu cha Eckernforde Tanga (2012-2019)Makamu mkuu wa chuo kikuu cha
Iringa(2015-2018 )vilevile ni muasisi na mwanachama,kiongozi na mlezi wa
jumuiya mbalimbali zinazojihusisha na lugha za fasini,jumuiya moja wapo
aliyoianzisha ni chama cha lugha na fasihi ya Kiswahili Tanzania
(CHALUFAKITA)
Dkt.Ponera
amesema kuwa kitabu hicho kinachoitwa Koja la Taaluma za Insia kwa
kifupi maana ya jina hilo ni taji au utungo uliosheheni maswala
mbalimbali yanayohusiana na taaluma za Insia.

Amefafanua
maana ya Insia ni neno lililotoholewa kutoka lugha ya kiarabu ins-yaani
mtu ama watu,hivyo insia linatoka kwenye neno Insia ambapo maana yake
ni kuhusiana na watu.
Amesema
kuwa kitabu hicho chenye kurasa 32ambazo zimegawanyika katika sura
10zenye mnyumbuliko tofautitofauti wameweza kuzalisha kopi 72 na wameuza
kwa mnada na kupata jumla ya shilingi million 2.5