Viongozi wa amcos waliotafuna fedha za wakulima shinyanga wakubali yaishe

SALVATORY NTANDU

Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa  Shinyanga imeokoa
Shilingi milioni 30, laki tano na elfu tatu miasita na hamsini kutoka
kwa Viongozi wa Vyama vya ushirika (AMCOS) waliofanya ubadhirifu wa
Fedha za Wakulima wa Pamba msimu wa Mwaka 2018/2019.

Akizungumza
na waandishi wa habari januari 14 mwaka huu Kaimu Mkuu wa (TAKUKURU)
Mkoa wa Shinyanga, Hussein Mussa alisema kuwa ofisi yake ilifuatilia kwa
kina madeni ya Wakulima wa Pamba wanaodai fedha zao kutokana na pamba
waliyouza kupitia AMCOS na kubaini kuwepo ubadhilifu wa fedha za
wakulima.

 Alisema
kuwa  Baada ya uchunguzi TAKUKURU  ilibaini kuwa AMCOS saba za Lugana,
Mwakipoya,  Ng’washinong’hela, Nyenze, Kalitu, Kweli Balimi na Ibadakuli
ndizo zinadaiwa fedha na wakulima wa pamba shilingi 109,497,130 licha
kuwa fedha hizo zimekwisha kutolewa na Kampuni za Ununuzi.

“TAKUKURU
ilibaini kuwa mpaka kufikia mwezi Desemba 2019 makampuni yaliyonunua
pamba mkoani Shinyanga yalikuwa hayadaiwi Fedha za Wakulima bali
walikuwa yanadaiwa ushuru wa AMCOS jumla ya Shilingi 890,105,580 alisema
Mussa.

Amefafanua
kuwa kuwa baada ya kubaini ubadhirifu huo Takukuru iliweza kuwakamata
baadhi ya Viongozi wa AMCOS waliofanya ubadhilifu wa fedha za Wakulima
na waliweza kurejesha kiasi cha Shilingi 30,503,650 fedha ambazo
zinatarajiwa  kugaiwa kwa Wakulima hivi Karibuni.


Viongozi wa AMCOS  ya Kweli Balimi ya Wilaya ya Shinyanga ambao
walirejesha Fedha walizokuwa wanadaiwa kiasi cha Shilingi 6,362,400
walikuwa wamezifanyia ubadhilifu na tayari fedha hizo zimeshatolewa kwa
Wakulima” alisema Mussa.

Aliwataka
wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano
kwa  TAKUKURU ili Kuhakikisha wanatokomeza  rushwa katika mkoa wa
Shinyanga.