Viongozi wa dini mkoani singida waja na maazimio saba uchaguzi mkuu

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini na Madhehebu mbalimbali Mkoa wa Singida,(aliyesimama)Hamis Muhamed Kisuke akiongoza kikao ambapo walizungumzia hali ya amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu na kuja na maazimo saba. (Picha na Rose Nyangasa).

Mkuu wa Mkoa  wa
Singida Dkt. Rehema Nchimbi  akizungumza
na  Kamati  ya Amani ya Viongozi wa Dini na
Madhehebu  mbalimbali Mkoa wa Singida ambapo
ameipongeza Kamati hiyo kwa kuamua 
kuhamasisha amani na utulivu kwenye 
kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu (Picha na Rose Nyangasa)

Wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Polisi wa MKoa wa Singida, Sweetbert Njewike (hayupo pichani) wakati akielezea majukumu ya jeshi hilo kwenye siku ya upigaji kura Oktoba 28, mwaka huu. (Picha na Rose Nyangasa).

Kamanda wa Polisi wa MKoa wa Singida, Sweetbert Njewike majukumu ya jeshi hilo kwenye siku ya upigaji kura Oktoba 28, mwaka huu. (Picha na Rose Nyangasa).

John Mapepele na Rose Nyangasa, Singida

Kamati ya Amani
na Dini mbalimbali   Mkoa wa Singida
inayojumuisha  viongozi wa madhehebu na
dini zote   imetoa tamko lenye maazimio
saba  kuelekea Uchaguzi Mkuu
utakaofanyika Oktoba  28, mwaka  huu huku 
ikiwaomba waumini wao kumtanguliza Mungu na Serikali  kusimamia 
amani na utulivu ili kuwapata viongozi bora watakaoingoza  nchi katika miaka mitano ijayo 2020 hadi 2025.

Akisoma
maazimio hayo, Mwenyekiti wa  Kamati hiyo
Shehe, Hamis Muhamed Kisuke amesema  miongoni mwa maazimio hayo ni  kuwaomba waumini wao kutenga siku tatu
kuanzia Ijumaa hadi Jumapili ya juma hili kwa ajili ya  kufunga na kuomba ili kuombea  uchaguzi upite  kwa 
amani na usalama.

Maazimio mengine  yaliyofikiwa kwenye kikao hicho ni pamoja
na  viongozi wa dini katika kipindi hiki
kudumisha  Amani, kutotumika   kwenye majukwaani ya siasa kushabikia  viongozi wa vyama vya siasa, kuhubiri Amani,

kuhimiza waumini wao kushiriki kupiga
kura na kuhimiza kufuata na kutii sheria za 
nchi ambapo  pia wamesisitiza
kuviacha vyombo  halali vilivyopewa
dhamana  ya kusimamia  uchaguzi huo vifanye kazi yake.

Mwakilishi wa
dini ya Kiislam (Baraza la Kiislam Tanzania) katika  Mkoa wa Singida Shehe, Issa Nassor amesema
Amani  ikitoweka  watakaoumia 
zaidi ni  watoto, wanawake,
wajawazito, wazee na watu wenye  mahitaji
maalum kwa kuwa  hawana  uwezo wa 
kukimbia  na kujitetea.

Aidha,  wamewataka wazazi  na walezi wa kila familia  kuwaasa 
vijana  kujiepusha  na kushawishiwa na watu wanaoitakia  mabaya 
nchi ya Tanzania ambapo ameongeza 
kwamba   baada ya  kupiga kura 
vijana warejee  nyumbani  kwa 
kuwa tayari Serikali imeshaweka 
vyombo  maalum kwa ajili  kuhesabu na kutangaza matokeo hayo.

“Historia
inaonyesha kuwa nchi zote duniani zilizopoteza amani ni nchi ambazo walilewa
amani, vilevile tukumbuke kupata amani ni mchakao wakati  kuvunja amani 
ni jambo rahisi  kabisa. Nawaomba
watanzania wenzangu  kutumia  vipande 
vyetu vya kupigia kura  kuwachagua  Viongozi bora” aliongeza  Shehe, Nassor

Mwakilishi kwa
upande wa wakristo, Askofu wa Kanisa la TAG mkoani Singida, Gasper Mdimi
amesema  amani  ya nchi ni jambo nyeti ambalo  linatakiwa 
kuchukuliwa  kwa uangalifu mkubwa
kwa kuwa  lina athari   pana 
kuanzia  kwenye  ngazi ya 
kaya  hadi taifa kwa ujumla  na kwamba 
Bibilia imefafanua  kuwa chanzo
cha Amani  ni  Mungu mwenyewe, Haki na Watu wanaomcha  Mungu.

Amefafanua kuwa  vitabu vyote 
vitakatifu  vinasisitiza
kutafuta  kuwa  na amani 
na watu wote ambapo   na kwamba
watanzania  wanatakiwa kupendana  katika kipindi hiki bila  kuangalia  
vyama vyao  vya  Siasa  
na kuiombea  nchi yao  ipate 
viongozi ambao  watailinda amani.

Pia
amesema   wakati  wananchi wanakwenda  katika siku za mwisho wa kuhitimisha zoezi la
kuwachagua viongozi   ni  muhimu 
kuzingatia kuacha kuongea  maneno
ambayo yatasababisha machafuko na 
uvunjifu wa amani.

Mwakilishi wa
Mhashamu Baba Askofu wa  Jimbo  Katoliki la Singida, Padre Padri Elia
Mnyakanka amesema Uongozi Bora ni tunu na zao 
la amani  na kwamba  ili kuwa na maendeleo na ustawi  kuanzia ngazi ya familia na taifa ni muhimu
kwa wananchi  kutafakari kwa kina  na kuwachagua viongozi wanaoweza kuilinda
amani.

Akitoa mfano
amesema katika taifa la Israel uongozi bora ulikuwa ni nyenzo ya
kuwafikisha  kwenye nchi ya ahadi kupitia
manabii mbalimbali ambapo kwa kufanya hivyo amani ilipatikana.

Amesema  viongozi wa dini wanapaswa  kuwapa elimu ya uraia waumini wao  ili kuwapa 
uwezo  wa  kuwachagua wagombea makini  kupitia ilani zao ambapo amesisitiza  kwamba uchaguzi wa haki na amani ndiyo njia
pekee ya kujitawala na kuleta amani katika nchi.

Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Singida,  Sweetbert
Njewike  amesema kwenye kipindi hiki  cha uchaguzi majukumu yao  ni pamoja na 
kutunza na kudumisha Amani, kusimamia utekelezaji wa sheria, kuzuia na
kubaini makosa ya jinai, kuwakamata wahalifu wanaohatarisha amani na
kuwafikisha katika vyombo vya sheria, kulinda 
mali za raia, kutoa ulinzi kwa maafisa na vituo, pia kuhakikisha hakuna
mtu anaye watishia wapiga kura na kuhakikisha usalama wa vifaa vya kupigia
kura. 

Mkuu wa Mkoa
Singida Dkt.Rehema Nchimbi amewashukuru viongozi hao kwa kuandaa mkutano  huu ambao umelenga kudumisha amani na
kuwahimiza wananchi washiriki kikamilifu kupiga kura  ili kuwa chagua viongozi bora.

Aidha Dkt.Nchimbi
amewataka Viongozi wa Dini kutotumika kuharibu amani na mshikamano ambao  upo kwa kipindi kirefu sasa hapa nchini
kutokana na kazi nzuri  ya kusimamia
amani hiyo iliyofanywa na Serikali.