Waamini waadiventista wasabato shinyanga mjini wamuaga mchungaji wao lazaro mbogo baada ya kuhamishwa utumishi

Na
Mapuli Misalaba, Shinyanga.

Waamini  Waadiventista Wasabato Shinyanga mjini  Jumamosi
Disemba 9,2023 wamemuaga mchungaji wao  Lazaro Mbogo baada ya kuhamishwa utumishi wake
kwenda  mtaa wa Katungulu Sengerema
Mkoani Mwanza.

Sabato
maalum ya kumuaga Mchungaji huyo imefanyika katika eneo la kanisa la Waadiventista
Wasabato Shinyanga mjini na kwamba, Mchungaji Mbogo amefanya utumishi wake kwa
muda wa takribani Miaka mitatu akiwa anatoa mafundisho  na huduma mbalimbali za kiroho kwa upendo na
furaha bila kuchoka.

Wakimuelezea
mchungaji Mbogo waamini Waadventista  wasabato wamesema kuwa alikuwa  mlezi mzuri ambaye alikuwa mstari wa mbele
katika kuchochea maendeleo na  kuwaimarisha kiimani.

Wamesema
wataendelea kumuenzi na kuyaishi yale mema na mazuri  aliyokuwa akiyafundisha kwao,na hivyo kumtakia
matashi mema na utumishi uliotukuka kule aendako kadri ya mapenzi ya mwenyezi
Mungu.

Kwa
upande wake mchungaji Lazaro Mbogo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru waamini
waadventista wasabato wa kanisa hilo, kwa ushirikiano wao na maombezi katika
utumishi wake kwa kipindi chote ambacho amekuwepo pamoja nao.

Hata
hivyo mchungaji Mbogo amewaasa kuendelea kutoa ushirikiano kwa mrithi wake
atakayekuja kuchukua nafasi yake, na kuwashukuru kwa zawadi walizompatia kwani
ni sehemu ya upendo mkubwa waliouonyesha kwake.

Waamini waadventina wasabato  Jumamosi
Disemba 09 mwaka 2023 wamemshukuru mungu kwa ajili ya zawadi ya mchungaji
lazaro mbogo katika kuwalea, kuwaongoza na kuwafundisha misingi ya imani,
ambapo wamemzawadia vitu mbalimbali ikiwemo nguo,chakula na fedha.

 

Mchungaji
 Lazaro Mbogo wa pili kutoka upande wa
kulia na viongozi mbalimbali wakiwa katika mabato maalum ya kumuaga mchungaji
huyo  Jumamos Disemba 9,2023.