Wachungaji watatu watupwa jela miezi sita kwa kujeruhi

NA MWANDISHI WETU
WACHUNGAJI watatu wa mifugo, wamehukukiwa kifungo cha miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki mbili kwa kosa la kujeruhi walinzi wa Msitu wa Hifadhi ya Kohondo uliopo kijiji cha Kihondo kata ya Doma wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Wachungaji hao waliohukumiwa ni  Sperwa Kishakwii, Daniel Babalai na Kashuma Kishaki.
Hukumu hiyo imetolewa Novemba 6/2019 na Hakimu Mussa Lilingani baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote ambapo Mahakama imewakuta na hatia wafugaji hao watatu.
Image result for Wachungaji wa ng'ombe
Wafugaji hao wanakutwa na hatia baada ya kuwashambulia na kuwajeruhi walizi wawili  wa  kamati ya Ulinzi wa hifadhi ya asili ya Msitu wa kijiji cha Kihondo, Emmanuel Willnely na Every Pius wakitaka kukomboa mifugo iliyokuwa ikishikiliwa.
Lilingani alisema hoja zilizo wasilishwa na watuhumiwa mahakamani hapo pamoja na mashahidi wao zilikosa uthibitisho ikiwemo kudai walipo fika kituo cha Polisi Doma waliwekwa Rumande bila Kuhojiwa,Umri walieleza kuwa chini ya Miaka 18 sambamba na maelezo kuwa siku hiyo ya tukio sio wao waliokuwa wakichunga mifugo iliyo kamatwa.
“Kufuatia ushahidi uliowasilishwa na upande wa walalamikaji pamoja na vielelezo vya upelelezi vya Jeshi la Polisi mahakama imejiridhisha na ushahidi ikiwemo vielelezo vya matibabu PF3, Fomu ya maelezo ya onyo toka kituo cha Polisi Doma pamoja na mkataba wa makabidhiano ya mifugo iliyo kamatwa wafugaji walikuwa na hatia” alisema.
 Hakimu Lilingani aliwaeleza washtakiwa hao kuwa mahakama imewatia hatiani na kuwataka kila mmoja kuieleza mahakama kama anautetezi wowote ili apunguziwe adhabu.
Mtuhumiwa namba moja Sperwa Kishakwii akatumia muda huo kuieleza mahakama kazi yake ni Mchungaji na anafanya kazi hiyo kama kibarua, hana baba wala mama anawadogo zake watatu na mmoja anaumwa, huku mtuhumiwa namba mbili yeye hakuwa na utetezi.
Katika utetezi wake mtuhumiwa namba tatu Kashuma Kishaki ameieleza mahakama kuwa kazi yake ni Mchungaji wa mifugo hana baba na mama yeka haoni, ana wadogo zake watatu, wawili ni wanafunzi na mmoja hana akili timamu hivyo yeye ndie tegemezi katika familia yao.
Mbali na utetezi huo Hakimu Lilingani alisema watuhumiwa wote wanahukumiwa kama watu wazima na kwakua wote hawajawai kuwa na kosa linguine kabla, adhabu ya mahakama ni kwenda jela miezi sita ama kulipa faini kiasi cha Shilingi Laki mbili kwa kila mmoja pamoja na Fidia ya Shilingi laki mbili kwa ajili ya waliojeruhiwa.
Pamoja na hayo mahakama imetoa amri kutaka fedha za adhabu zilipwe ndani ya siku 45 na kiasi kingine cha fedha za fidia zilipwe ndani ya siku tano baada ya fedha za mahakama.
 
Kwa mujibu wa hakimu Lilingani Rufaa ya kesi hiyo ipo wazi ndani ya kipindi ca siku 30 huku nje ya mahakama walalamikaji wakieleza kuto ridhishwa na hukumu iliyo tolewa.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *