Na WAMJW-Dar es Salaam
Serikali
imepokea msaada wa shilingi bilioni 14.9 kutoka Global Fund, Airtel
Tanzania, Rotary Club Tanzania ambazo sehemu kubwa zitatumika kununua
vifaa kinga kwa watumishi wa afya na vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia
wagonjwa wenye maambukizi ya COVID-19.

Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
ameyasema hayo leo wakati akipokea msaada wa fedha na lita 1,250 za
vitakasa mikono ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za
kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Ummy amefafanua kwamba Global Fund imetoa shilingi bilioni 14, Airtel
Tanzania shilingi milioni 700 na Rotary Club Tanzania shilingi milioni
250.

“Tumepokea
shilingi bilioni 14 kutoka Global Fund, shilingi bilioni 9.6 tumezitoa
kwa ajili ya kununua vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa Afya, lakini
pia fedha zilizotolewa na Airtel na Rotary Club Tanzania tutazielekeza
huko. Kipaumbele chetu ni kuwalinda watumishi wa afya,” amesema Waziri
wa Afya, Ummy Mwalimu.

“Natumia
fursa hii kuwashukuru watumishi wa afya ambao wamekuwa wakijitoa usiku
na mchana katika kutoa huduma kwa watu waliopata maambukizi ya virusi
vya Corona (Covid-19) pamoja na wale wahisiwa.

“Kipaumbele
cha Serikali ni kuwalinda watumishi wa Afya kwa kununua vifaa kinga
kwani fedha tulizozipata hapa tutazielekeza kwenye ununuzi wa vifaa
kinga. Niendelee kuwaisistiza Watumishi wa Afya wazingatie miongozo ya
magonjwa ya kuambukiza,” Amesema Waziri Ummy .

Amesema
watumishi wa afya ambao wamepatiwa mafunzo katika vituo vya kutoa
huduma kwa wenyr maambukizi ya ugonjwa huo, hakuna aliyepata maambukizi
kwa kuwa wanazingatia miongozo ya Serikali ya kutoa matibabu kwa
wagonjwa wa Covid-19 pamoja na miongozo ya magonjwa ya kuambukiza.

amesema ushiriki wa kila mdau katika mapambano dhidi ya maambikizi ya
virusi vya Corona ni muhimu na kwamba msaada uliotolewa na kampuni hizo
ni mkubwa katika mapambano ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

“Napenda
kurudia tena kwa niaba Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, nawashukuru Airtel Tanzania, Serengenti Breweries na Rotary
Club kwa hiki mlichotupatia. Asanteni sana,” amesema Waziri Ummy.

Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Airtel Tanzania, Bw. Gabriel Malata
amesema Airtel Tanzania imetoa shilingi milioni 700 ikiwa ni sehemu ya
kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na janga la Corona.

“Sisi
bodi ya wakurugenzi wa Airtel na kwa niaba ya Airtel Tanzania,
tunatambua juhudi za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Corona,
lakini pia tumejitathimini na kutambua kuwa sisi kama Airtel hatuwezi
kuendelea bila kuwepo watu wanaotumia huduma zetu. Watu hawa ndio mtaji
wa Kampuni,” amesema Bw. Gabriel.

Mkurugenzi
wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengenti, Bw. John Wanyancha amesema
kuwa kampuni hiyo imetoa lita 1,250 ya vitakasa mikono nyenye thamani
ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za
kupambana na maambukiza ya virusi.

Mwenyekiti
wa Rotary Club, Bi. Agnes Batenga amesema Rotary imetoa shilingi
milioni 250 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa homa ya mapafu
(COVID-19).

“Shilingi
milioni 183 zitatumika kutoa msaada wa vifaa vya kujikinga (PPE), vifaa
vya maji safi ambavyo vitasambazwa katika vituo maalumu vya kuhudumia
wagonjwa wa Corona jijini Dar es Salaam, Hospitali ya Amana, Zanzibar,
Hospitali ya Mawenzi na Hospitali ya Mount Meru,” amesema Bi. Agnes.

Amesema shilingi milioni 67 zitatumika katika kutekeleza miradi ya kudhibiti ugonjwa wa Corona nchini kupitia Club za Rotary.