Wafanyakazi wanawake tcra kanda ya kaskazini watembelea shule ya weruweru na kutoa elimu.

Wafanyakazi na wake wa wafanyakazi wa TCRA katika picha ya pamoja walipokwenda kutoa elimu ya matumizi bora ya mtandao Weruweru
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Weruweru wakiwa katika picha za pamoja  

Eng. Emelda wakati akiwasilisha mada ya matumizi bora ya mitandao kwa wanafunzi wa Sekondari Weruweru
Eng. Emelda Salum akiongea na wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya weruweru iliyopo mkoa wa Kilimanjaro



Na.Vero Ignatus,Arusha
Katika
kusheherekea siku ya wanawake duniani 8/3/2020 wanawake wanaofanyakazi
ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Kaskazini
wameamua kutumia maadhimisho hayo kutoa elimu ya matumizi bora ya
mitandao ya kijamii kwa wanafunzi wa shule ya wasichana Weruweru iliyopo
mkoani Kilimanjaro.

 Akizungumza na wasichana hao wa kidato cha tano na sita mkuu wa kanda wa Taasisi hiyo Eng. Emelda Salum alisema
lengo la kutoa elimu hiyo ni kuwaelimisha wasichana ambao wako mbioni
kumaliza masomo na watakapo anza kutumia mitandao ya kijamii kwamba
watumie kwa ufasaha kwani wao ndio waathirika wakubwa wa madhila ya
mitandaoni.

 “Tumeona
tuwape wasichana zawadi itakayo wasaidia kwenye maisha yao ya kesho
watakapoanza kutumia mitandao kwa kuwafundisha juu ya sheria ya makosa
ya mitandao na matendo yatakayo washushia hadhi au hata kushindwa
kuajirika” alisema Eng. Emelda. 

 Aliongeza
kuwa kampuni nyingi hivi sasa mbali na kuangalia ufaulu wa kwenye vyeti
ili wakuajiri wanaenda mbali zaidi kuangalia hata kwenye account za
mitandao ya kijamii namna mhusika anavyo itumia na kwamba kwa wanafunzi
hao ambao mbioni wanakwenda kumaliza shule ni vyema wasiingie kwenye
mkumbo huo. 

 Anzirani Ibrahim mwanafunzi
wa kidati cha tano (EGM), mara baada ya kupata somo hilo alisema kuna
vijana wanaoathirika na madhila ya mitandaoni kwa kutokujua hivyo kwa
upanda wao wanaona ni nafasi ya kipekee kupata elimu hiyo.

 Naye dada mkuu wa shule hiyo Irene Siami kidato cha sita (PCB) maarufu kama President aliahidi kutokuwa wachoyo wa kuelimisha wengine juu ya matumizi bora ya mitandano.

 Mkuu wa shule hiyo Mwl. Rosalia Frimin aliwapongeza
TCRA kwa kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi wapatao 750 wa kidato cha tano
na sita, mbali na Computer 10 pamoja na mtambo wa Internet waliopewa
hivi karibuni.