Wakazi kata ya ramadhan wamsaidia mkandarasi kusogeza umeme majumbani mwao

Na Joctan Agustino, Njombe

Wakazi wa mtaa wa Itulike kata ya Ramadhani halmashauri ya
mji wa Njombe wameshindwa kuzuia hisia zao na kuamua kushiriki katika
zoezi la uchimbaji mashimo ya kusimika nguzo za umeme pamoja na
kusafisha njia za kupitisha nguzo za umeme ili kuharakisha zoezi la
usogezaji wa huduma hiyo ambayo hawajaipata tangu uhuru licha ya mtaa
wao kuwepo katika kata ya mjini.


Wakazi hao akiwemo 

Michael Jacob ambaye ni mkiti wa mtaa  pamoja na Angela Exavel  wanasema
wamelazimika kushirikiana na jopo la mafundi wa Tanesco kusogeza vifaa
vya ujenzi wa mradi, uchimbaji wa mashimo ya nguzo pamoja na usafishaji
wa njia za umeme ili kuipunguzia mzigo mafundi umeme ambao wamefika kwa
ajili ya kukamilisha zoezi la uunganishaji wa nishati hiyo.


Wanasema
ujio wa nishati ya umeme katika eneo hilo utaharakisha maendeleo
kwasababu kwa kipindi kirefu wamekuwa wakifata umbali wa zaidi ya km 10
hadi 15  mashine za mafuta kusaga huku pia viwanda kadhaa kikiwemo cha
maziwa vikishindwa kufanya kazi ipasavyo kutokana na ukosefu wa huduma
ya umeme

Ujio wa timu ya mafundi iliyoweka kambi mtaa wa Itulike
ikiongozwa na Naftali Kiula ambaye ni mkandarasi kutoka kampuni tanzu ya
tanesco ya Electrical Transmision and Distribution Company ITDCO
unawafanya wananchi kuhoji ukombo wa utekelezaji wa mradi huo jambo
ambalo linatolewa ufafanuzi na mkandarasi.

Wakati ufafanuzi
huo ukitolewa nae katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe
ameshiriki katika uchimbaji wa mashimbo ya kusimika nguzo anasema
wamepata shida kwa kipindi kirefu ya kufata huduma umeme vijiji jirani
wakiwa na mizigo kichwani na kwamba ujio wa nishati hiyo utachagiza
maendeleo katika eneo hilo linalotambulika kama bustani ya tunda la
parachichi.