Watumishi wa umma watakiwa kuendana na wakati kiutendaji

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri akielezea historia fupi ya Mkoa
wa Tabora kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini
Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg walipomtembelea ofisini kwake jana kabla ya
kutembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora kwa lengo la kuona
maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania
na Sweden mwaka 1970. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora
Mjini, Mhe. Kitwala Komanya.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe.
Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg kuingia
Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo
ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden
mwaka 1970. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri
na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakiungana na
wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora na
wageni wengine kucheza muziki uliokuwa ukitumbuizwa na bendi ya Msange JKT wakati
wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora jana kwa
lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa
Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mtendaji
Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.
Mkufunzi Msaidizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bw. Alex
Massengo akiwaonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora,
Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg
matukio mbalimbali katika picha yakiwemo yanayohusu ushirikiano wa Serikali ya
Tanzania na Sweden katika kujenga Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora
wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora jana
kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho.
Mkuu wa Idara ya Uhazili,  Chuo cha
Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bw. Given Simkwai akiwaonyesha Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden
nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg umuhimu wa 
matumizi ya hati  mkato wakati
wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora jana kwa
lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa
Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970.
Meneja wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bi. Felister
Akonaay akiwaonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini
Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg kibao kinachoonyesha ushirikiano wa Serikali ya
Tanzania na Sweden katika kujenga Chuo cha Utumishi wa Umma, Tawi la Tabora
wakati wageni hao walipotembelea Chuo hicho jana kwa lengo la kuona maendeleo
yake


Na Mary
Mwakapenda, Tabora

Watumishi
wa Umma nchini wametakiwa kubadilika kiutendaji ili kuendana na kasi ya
mabadiliko mbalimbali yanayotokea hivi sasa duniani kwa lengo la kuliletea
taifa letu maendeleo.

Hayo
yalisemwa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara yake ya kikazi
na Balozi wa Sweden nchini Tanzania
, Anders Sjoberg iliyolenga kuangalia maendeleo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya
Tabora kilichojengwa mwaka 1970 kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na
Sweden.



Mhe.
Dkt. Mwanjelwa amesema hivi sasa kila kitu kinabadilika duniani ikiwemo uchumi,
maisha na teknolojia, hivyo watumishi wa umma hawana budi kubadilika kulingana
na wakati uliopo, kwa mantiki hiyo ni lazima wawe wabunifu na kuacha kufanya
kazi kwa mazoea hatimaye  taifa liweze
kunufaika na mchango wao.

“Kama
katika sekta binafsi wanafanya kazi ipasavyo kwanini katika Sekta ya Umma
tushindwe? ikizingatiwa kuwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu  wanahitaji huduma kutoka serikalini na
waliopewa dhamana ya kuwahudumia ni sisi,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa alihoji na
kuongeza kuwa, ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi makini wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
inasisitiza na kuiishi kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu ili watumishi wa umma wawe na
tija kwa taif
a.

Aidha,
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewasisitiza watumishi na wanafunzi wa Chuo cha Utumishi
wa Umma kila mmoja kwa nafasi yake kutekeleza wajibu wake ipasavyo  ili kutimiza malengo waliyojiwekea.

“Ukiwa
mwanafunzi soma kwa bidii na mtumishi fanya kazi kwa bidii ili kutimiza ndoto
yako kwani Serikali inataka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kiendelee kutoa
mchango katika maendeleo ya taifa na kuwa mfano bora wa kuigwa na vyuo vingine”
Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliongeza.

Akitoa
salamu za Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri
amemshukuru Naibu Waziri na Balozi Sjoberg kwa ujio wao kwani unaendelea
kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Sweden ambao ulianza tangu Serikali
ya Awamu ya Kwanza mpaka sasa.

Mhe.
Mwanri amewaasa wanafunzi wa chuo hicho kutumia vema ujuzi watakaoupata kwa
manufaa yao na maslahi ya taifa na kuongeza kuwa chuo hicho kina historia ya
kutoa viongozi bora huku akitoa mfano wa baadhi ya viongozi waliosoma hapo na
kupata mafanikio makubwa akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu na Mke wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Hayati Robert
Mugabe, Mama Grace Mugabe.

Kwa
upande wake, Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg a
lishukuru
kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kuwaasa wanafunzi na watumishi wa chuo hicho
kutekeleza wajibu wao ipasavyo, na hakusita kupongeza juhudi zinazofanywa na
Serikali ya Tanzania

za kukiendeleza chuo hicho.

Ziara
hiyo ilitoa fursa kwa viongozi hao kutembelea maktaba ya kumbukumbu, maktaba,
chumba cha Kompyuta, darasa la kupiga chapa
, mabweni ya wanafunzi na
jengo jipya la utawala linalojengwa kwa fedha za ndani ambalo  limekamilika kwa asilimia 94 kwa gharama ya
shilingi bilioni 2.7.