Raila Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya |
BAADA ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga kusema
kuwa Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anashauriwa vibaya kuhusu mlipuko
wa ugonjwa wa Corona, wasomaji mbalimbali wamepingana vikali na kauli hiyo na
kusema kuwa Rais Magufuli yuko sahihi na aachwe na msimamo wake.
Wakichangia katika ukurasa wa kituo cha redio cha BBC ambacho
ndicho kilichorusha taarifa hiyo baada ya kufanya mahojiano na kiongozi huyo wa
Kenya, mmoja wa wakenya amesema Raila hana jambo ambalo anaweza kumshauri Rais Magufuli
katika CORONA kwa kuwa Tanzania ndio nchi pekee inayoonyesha njia ukanda wa Afrika.
Mchangiaji mwingine anayejiita, JPM forever ameandika kuwa, “BBC
mtuache sisi ndio wapiga kura wake, nyie inawauma nini fanyeni yanayowahusu ya
JPM mtuachie sisi na mwaka huu tunamchagua tena, ili iwaume zaidi fungeni midomo
sisi watanzania tunamkubali Rais wetu na tupo nae katika kipindi ichi sio yeye
aliyeleta corona mngekuwa wa maana mngejadili aliyeileta hii corona duniani “.
Aliongeza, “Kama habari hamna njooni niwape habari za yesu
anavyoipigania Tanzania na alivyokaribu na Rais wetu, hii nchi inaongozwa na Mungu
na Rais wetu anaongozwa na Mungu na pia wananchi wake tunaongozwa na Mungu sisi
atumtegemei binaadam katika kuendesha taifa letu bali tunamtegemea Mungu kila
mtu kwa imani yake, kwa hiyo kama mnataka kutuchonganisha watanzania sio
wajinga na ndio maana hizo comment zote zinawakandamiza nyie BBC na kwa
waandishi wenu wenye chuki na taifa letu,”.
Waliomba kiongozi huyo wa Kenya kujadili masuala
yanayoendelea nchini kwake na kuiacha Tanzania ikiendelea kupambana na hali ya
ugonjwa huo ambao kihalisia haupo nchini baada ya Rais kuamua kufanya maamuzi
magumu.
Tangu kulipoibuka kwa ugonjwa wa CORONA mapema machi mwaka
huu, tayari maelfu ya watu duniani wamefariki duniani huku ugonjwa ukiendelea
kusambaa maeneo mengi Zaidi duniani.