Wanafunzi chuo kikuu cha dar es salaam kuandamana desemba 19

Serikali
ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) imetoa saa 72 kwa
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutoa mikopo kwa
wanafunzi waliokosa, vinginevyo wanafunzi watakutana nje ya ofisi za
bodi hiyo zilizopo Mwenge Dar es Salaam Desemba 19, 2019.



Taarifa
iliyotolewa jana Jumapili Desemba 15, 2019 na Waziri wa Habari na
Mawasiliano wa Daruso, Judith Mariki ilisema wamefikia uamuzi huo baada
ya changamoto ya kukosekana kwa mikopo kwa wanafunzi wengi wa mwaka wa
kwanza tangu chuo kifunguliwe huku baadhi ya wanafunzi wanaoendelea
wakikatwa fedha zao.

Mariki
alisema baada ya juhudi kubwa ya kufuatilia na mazungumzo kugonga
mwamba, serikali imefanya mazungumzo ya ndani kwa ndani iliyojumuisha
mihimili mitatu ya serikali hiyo.