Wananchi nyakunguru tarime wamlilia rais magufuli ulipwaji wa fidia

Na Mwandishi wetu Tarime.

Mmoja wa wananchi akizungumza katika mkutano huo 

Wananchi wa kijiji cha Nyakunguru Kata ya Kibasuka Wilayani Tarime Mkoani Mara wameiomba serikali kuingilia kati ili waweze kulipwa fidia katika maeneo ambayo tayari yamefanyiwa tathimini tangu mwaka 2013.

Wananchi hao wamedai kuwa Maeneo ambayo tayari yamefanyiwa uthamini ni phase ya 24 na 34 lakini mpaka sasa miaka saba hawajalipwa hivyo wameiomba serikali kuingilia kati suala hilo mgodi wa Uchimbaji wa mawe ya Dhahabu Barrick North Mara waweze kulipa.

 Magige Ghati ni mmoja wa wananchi akiongea katika kikao cha wananchi alisema kuwa wathamani wakiwemo viongozi kutoa Wizara ya Madini na Ardhi walipita kijijini hapo na kufanya tathimini na kuwambia wananchi hao kupisha maeneo hayo lakini mpaka sasa hawajalipwa.

“Uthamini ulifanyika tangu mwaka 2013 mpaka sasa imefika miaka saba pia phase ambazo zilipaswa kulipwa zilikuwa sita lakini nne zimelipwa tayari  na phase ambazo zimebaki ni phase mbili ambazo ni phase ya 24 na 34 tunaomba serikali ya awamu ya tano isikilize kilio chetu” alisema Ghati.

Penina Mwita aliongeza kuwa kutolipwa fidia hizo kwa wananchi hao baadhi yao wameathilika kisaikorojia pamoja na kushuka kwa uchumi na wakati mwingine kushindwa kulipa karo za wanafunzi kwani kipato chao kimeshuka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Nyakunguru  Chacha Makuri alisema kuwa Wananchi wamekuwa wakipiga simu mara kwa mara kuhusua suala la serikali kwa kushirikiana n mgodi wa uchimbaji wa mawe yenye dhahabu North Mara kulipa fidia ili wananchi waendelee na shughuli zao lakini chakushangaza mpaka sasa hakuna taarifa juu ya malipo hayo.

 “Leo hiki kikao cha wananchi wameamua kupaza sauti ili serikali iweze kuwasikiliza kwa sababu miaka mingi hatulipwi lakini wenzetu vijiji jirani wamelipwa”  alisema Makuri.

 Esther Charles alisema kuwa yeye ameolewa kijijini hapo mpaka sasa mmewe alifariki akidai malipo ya fidia hivyo sasa serikali ione haja kubwa ya kuwalipa ili wajukuu wake wawezekwenda shule.

Vilevile Bauru Timas ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nyakunguru alisema kuwa maeneo ambayo alikuwa akitumia kujiingizia kipato kwa kuuza Matunda yalishapelekwa kwa mwekezaji baada ya kufanyiwa tathimini mwaka 2013 lakini mpaka sasa hajalipwa hivyo amesisitiza serikali kusikiliza kilio cha wananchi hao.

  Akiongea kwa niaba ya srikali mkuu wa wilaya ya Tarime Mhandisi Mtemi Msafiri alisema kuwa changamoto kubwa ni wananchi hao kutegesha mazao jambo ambalo linachelewesha zoezi hilo.

Mkuu wa Wilaya alisisitiza wananchi hao kuendelea kufuata sheria na taratibu za Nchi hususani linapokuja suala la malipo nakuongeza kuwa kwa sasa wanaendelea na malipo kijiji cha matongo hivyo wananchi waendelee kuvuta subira.

“Unakuta mtu anaeneo moja lakini analikatakata vipande nakuwagawia wengine pia wanapanda kila aina ya mazao Mitipela, Mikonge Alovera na kila kitu sasa lazima tukatumiea watalaamu wa masuala la ardhi ili kila mwananchi apate haki yake” alisema Mtemi.