Wananchi rufiji kunufaika zaidi na mradi wa umeme stiglers

 

Na Mwandishi wetu

Wananchi wa Wilaya ya Rufiji mkoa Pwani ,wamemshukuru Rais John Magufuli baada ya kuanza kunufaika na mradi mkubwa wa bwawa la kuzalisha umeme  wa Stiglers Gorge kwa kupata sh 5 bilioni kila mwaka na ajira.

Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa (CCM) alisema ujenzi wa mradi huo umekuwa na manufaa makubwa kwa wilaya hiyo .

Alisema kwa Sasa rufiki itakuwa inapata fedha hizo sh 5 bilioni Kama Kodi ya huduma na kampuni iliyopewa zabuni ya mradi huo.

Alisema fedha hizo zinatarajiwa kutumika kuboresha maisha ya Wananchi wa Rufiji katika miradi mbalimbali ya afya,elimu,maji na barabara lakini pia kutoa mikopo kwa akina mama na vijana.

Alisema wilaya hiyo ambayo  sehemu kubwa ya mradi wa huo wa  umeme pia vijana zaidi ya wengi wamepata ajira.

“Tunamshukuru Sana Rais John Magufuli kwa kukubali kuendeleza mradi huu mkubwa wa umeme wa  kihistoria ambao unakwenda kubadili kabisa maisha ya watanzania”alisema

Alisema mradi huo ukikamilika bei ya umeme itashuka Sana nchini lakini pia Taifa litauza nje umeme na hivyo kuimarika kiuchumi.

“Kwa rufiji tunatarajia kujengwa  viwanda vya kisasa lakini miji itakua kiuchumi kutokana na umeme wa uhakika”alisema

Alisema pia kupitia mradi huo wanatarajia kuimarika kilimo Cha umwagiliaji katika wilaya hiyo kwani ndio ambayo hupokea maji mengi kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mchengerwa alisema wananchi wa Rufiji kwa kutambua kazi nzuri ya Rais John Magufuli kwa Mara ya Kwanza wamempa kura nyingi Sana sambamba na kurejesha Mbunge wa CCM na Madiwani tofauti na miaka ya nyuma.