Wanavyuo watakiwa kujijengea nidhamu ya matumizi ya fedha wanazopewa na bodi na wazazi

 

Mkamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda
(wa pili kutoka kushoto) Akizungumza na Washindi wa mashindano hayo na
wanafunzi wengine walioshiriki kwenye hafla hiyo, Kushoto ni Meneja wa
CRDB tawi la SUA Isabela Kitila.


Mshindi
wa kwanza kwenye mashindano hayo ambaye amepatiwa laptop Megan Manase
Mushi akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washindi wenzake.


Meneja
wa Benki ya CRDB tawila la SUA Isabela Kitila akieleza namna washindi
hao walivyopatikana kabla ya zoezi la utoaji wa zawadi.


Mkamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda
(Katikati) akimkabidhi mshindi wa Simu Abeid Naftari Mtemi simu yake na
kushoto ni Meneja wa CRDB tawi la SUA.



Mkamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda
(Katikati) akimkabidhi Mshindi wa laptop Megan Manase Mushi laptop yake
na kushoto ni Meneja wa CRDB tawi la SUA.



Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Upande wa Taaluma
Prof. Maulid Mwatawala (mwenye tai nyekundu) akiwa Mshauri wa wanafunzi
SUA Bwana Pure Mulshabi na viongozi wengine wa SUA na CRDB wakati wa
afya hiyo.


Washindi
wa shindano hilo wakiwa kwenye picha ya Pamoja na mgeni rasmi katika
hafla hiyo ambaye ni Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA
Prof. Raphael Chibunda pamoja na Viongozi wa CRDB na Viongozi wa
Serikali ya Wanafunzi SUA yaani SUASO.



Wanafunzi na viongozi wa wanafunzi SUASO wakifuatilia tukio hilo la utoaji wa zawadi kwa wenzao.




Na: Calvin Gwabara – Morogoro.


Makamu
wa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael
Chibunda amewataka Wanafunzi wa Chuo hicho kufungua akauti katika
Taasisi za Kifedha ili kuweza kuwajengea nidhamu ya fedha wanazo zipata
kutoka bodi ya mikopo na kwa Wazazi.


Ushauri
huo ameutoa wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi
watatu ambao wameshinda zawadi za Tanakilishi mpakato yaani (LAPTOP
mbili na Simu janja moja zilizotolewa na Benki ya CRDB tawi la SUA
kutokana na kufanya miamala mingi kupitia akauti zao za SCHOLAR ACCOUT.


“Mimi
niwapongeza kwa kuweza kushinda, nyinyi ni vijana lakini mkae mkijua
ujana unapita na majukumu yanazidi kuongezeka ni vizuri kujiwekea
utamaduni wa kutumia taasisi za kifedha wale ambao mmeamua kwenda CRDB
kungua hizi akauti nawapongeza sana matumiani yangu ni kwamba
hitawajengea nidhamu ya matumizi mazuri ya fedha mnazo zipata”Alisema
Prof .Chibunda.


Prof.
Chibunda fedha amesema ambazo wanazipata kutoka kwenye bodi ya Mikopo
ya Elimu ya Juu, amewakumbusha kuwa ni kweli zile ni za mkopo na mkopo
siku zote unapaswa utumike kwa tahadhali na kwa malengo ambayo
yamekusudiwa hivyo wawe makini kwenye matumizi na kukumbuka kuzirudisha
wamalizapo chuo ili zisaidia Watanzania wengine.


Ametumia
pia nafasi hiyo kuwakumbusha Wanafunzi wote kuchukua tahadhari katika
wakati huu ambao jamii serikali na wataalamu wa afya wanakumbusha
kuchukua tahadhari zote za maambukizi ya Ugonjwa wa COVID 19 kama
ambavyo inashauriwa na wasifanye mzaha maana Chuoni kuna wanafunzi
wengi.


“Sisi
kama Chuo tumeweka maji ya kunawa kila kona ya Chuo chetu ili Wanafunzi
waweze kupata huduma za kunawa mikono na tunaomba msipuuze naweni
mikono na msione aibu kuvaa barakoa vaeni kama mnazo ili mjikinge nyinyi
na na kuwakinga wenzenu pia|” Alisisitiza Prof. Chibunda.


Kwaupande
wake Meneja wa Benki ya CRDB tawila la SUA Isabela Kitila amesema CRDB
imweza kubuni na kuja na akauti hiyo ya SCHOLAR ACCOUT ili kuweza
kumsaidia Mwanafunzi kipindi anapokuwa Chuoni katika kipindi chake cha
masomo.


“Hii
akauti haina makato ya mwezi kwahiyo mwanafunzi anapofanya miamala yake
anakuwa huru kwasababu tunajua Mwanafunzi anakuwa na mambo mengi
vilevile tunafahamu uchumi wa Mwanafunzi ndio maana tumeweza kuja na hii
ili kuweza kupunguza chaji za mwezi za makato, Akauti hii pia
Mwanafunzi anaweza kuitumia mahali popote ata akiwa tayali ameajiriwa”
Alifafanua Isabela.


Akizungumzia
manufaa yatokanayo na akaunti hiyo ya SCHOLAR Isabela amesema kuwa
inaweza kumsaidia Mwanafunzi kupata mkopo wa awali kupitia Benki ya CRDB
ili aweze kutatua changamoto zinazomkabili na kuweza kulipa pale
atakapo pata mkopo kutoka Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu.


“Vilevili
utaweza kupata huduma mbalimbali kupitia benki yetu ya CRDB kama Simu
benking,internet benking, na kuweza kufanya manunuzi ya mtadaoni ukiwa
Chuoni na unamkopo ni vizuri kujiifadhia fedha kidogo unapo maliza Chuo
anagalau na wewe unakuwa na fedha ambazo utaweza kuanzia maisha mtaani
”.Aliongeza Meneja huyo wa CRDB Tawi la SUA.


Akiongea
kwa niaba ya wanafunzi ambao wameshinda zawadi hizo Megan Manase Mushi
wamesema kupata Tanakilishi (Laptop) zitawasaidia katika kufanyia
shughuli mbalimbali za kimasomo maana hawakuwa nazo kabisa hivyo CRDB
imekuwa mkombozi katika kuwapatia vitendea kazi hivyo.


Paia
wamewataka Wanafunzi wengine kujiunga na Benki ya CRDB kwani kwani
imekuwa ina huduma nyingi nzuri kwaajili ya wanafunzi ambazo
zitawasaidia katika kutunza fedha na kuzitumia vizuri pindi
wanapozihitaji maana kila mahali sasa wanapatikana.