Taec:mionzi ina faida kubwa na siyo madhara peke yake

Profesa Lazaro Busagala,Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu ya nchini (TAEC) akizungumza na washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa usalama wa mionzi yaliyofanyika Makao makuu ya Tume hiyo Jijini Arusha.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ya siku tano kutoka Serengeti Breweries mafunzo ya usimamizi wa usalama wa mionzi yaliyofanyika Makao makuu ya Tume hiyo Jijini Arusha.
 Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya  mafunzo ya usimamizi wa usalama wa mionzi yaliyofanyika Makao makuu ya Tume hiyo Jijini Arusha.  Mgodi  wa Bulyahulu
 Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TAEC Dkt.Justine Ngaile akitoa kutoa elimu kuhusiana na mionzi madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mionzi 
Mafunzo yakiendelea juu ya kuhusiana na mionzi madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mionzi

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TAEC Dkt.Justine Ngaile akiwa katika picha ya pamoja siku ya ufunguzi rasmi ya mafunzo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu ya nchini (TAEC) Profesa Lazaro Busagala akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo


Na.Vero Ignatus,Arusha

Imeeelezwa
kuwa Teknolojia ya Nyulia na mionzi kwa ujumla ina faida kubwa katika
kuongeza uchumi wa Taifa ikitumiwa vizuri na siyo kwamba ina madhara
katika afya ya binadamu pekee kama vile watu wengi wanavyofahamu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu ya nchini (TAEC) Profesa Lazaro Busagala kwamba teknolojia
hiyo imeweza kutumika kwenye kilimo,Afya,kuhifadhi vyakula,viwandani
hivyo ni vyema jamii itambue kuwa teknolojia karibia zote hapa duniani
zina faida na hasara zake.

”Teknolojia
ya Nyuklia na mionzi haina hasara bali ina faida kubwa kwani Teknolojia
hiyo ya nyuklia  imeweza kuleta mbegu bora zaidi za mpunga ambayo
imetoka mwaka 2019”

Amesema
Teknolojia hiyo ya mionzi  inaweza kuwapa Watanzania chakula kilicho
salama zaidi  kwasababu mionzi haibaki kwenye chakula ni tofauti na
kuweka kemikali kwaajili ya  kuhifadhia vyakula
“Hii
ni sawasawa na piga tochi ukizima tochi ule mwanga haubaki kwenye
chakula hivyo ni salama zaidi kuliko ambavyo unaweza ukachukua kemikali
ukapitisha kwenye kiwanda ukahifadhi vyakula hivyo

Profesa Busagala 
alisema kuwa TAEC itaendelea kuboresha maeneo ambayo yanaonekana
yanahitai maboresho zaidi sambamba na kutoa ratiba ya mwaka ambapo
tayari imekwisha kuanza mwaka huu 2020 na kuboresha namna ya kuwasikiana
na Taasisi mbalimbali  

Akifunga
mafunzo ya yaliyoendeshwa kwa siku 5 juu ya usimamizi wa usalama wa
mionzi kwa wafanyakazi wanaotumia vifaa vitumiavyo mionzi migodini
viwandani na kwa watengenezaji wa vifaa vya mionzi vya
hospitalini,waitumie elimu hiyo kwa manufaa ya jamii inayowazunguka

Awali akifungua mafunzo hayo juzi feb 18 Kaimu mkurugenzi mkuu wa TAEC Dkt.Justine Ngaile alisema lengo kuu ni kutoa elimu kuhusiana na mionzi madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mionzi.

Alisema
kuwa sheria inayosimamia udhibiti wa matumizi salama ya mionzi namna
bora ya kujikinga dhidi ya madhara ya mionzi(Radiation protection
Principals )kwa kuzingatia kanuni za ulinzi wa mionzi katika kuhakikisha
usalama wa watumiaji wa watengenezaji wa mashine za Midaki (X-Ray
Baggage Scanner)

Dkt.Ngaile alisema
kuwa mafunzo hayo yatawawezesha washiriki kupata elimu juu ya matumizi
salama ya vyanzo vya mionzi ili kujikinga na madhara yanayoweza
kusababishwa na mionzi katika maeneo yao ya kazi.

Aidha
mafunzo hayo yaliweza kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 16 kutoka
migodi ya Bulyahulu ,Kampuni ya soda ya Cocacola,Serengeti Breweries
,watengeneaji wa vifaa vya mionzi (Repair and Maintenance ofa Nuclear
Equipments)Hospitali ya Bugando ,Oceanic Pacific na Archelis.

Sambamba
na hayo Majukumu ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni pamoja na kudhibiti
matumizi salama ya mionzi nchini,kuhamasisha na kupanua matumizi salama
ya Teknolojia ya Nyuklia na kutoa ushauri na taarifa mbalimbali za
Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia