Na Clavery Christian Kagera
Jumla ya watoto 147 wamenyanyaswa na walezi pamoja na wazazi wao katika kipindi cha mwezi june hadi july mwaka huu 2020, wilayani missenyi Mkoani kagera.
Akizungumza na mwandishi wa APC Blog ofisini kwake mapema leo,mwenyekiti wa wasaidizi wa kisheria wilayani humo bwana Merikyoli Salapion amesema kuwa kati ya watoto hao wa kike ni 64 na wa kiume ni 78.
Ameongeza vitendo hivyo vimeripotiwa na majirani wa watoto hao ambao wameweza kutoa taarifa za siri katika ofisi za wasaidizi wa kisheria pamoja na ustawi wa jamii.
Ameongeza kuwa,ofisi hizo zimeweza kuwasaidia walezi wa watoto hao kwa kuwashauri kuacha unyanyasaji huo ambao miongoni mwao ni pamoja na kuwanyima matumizi.