Afisa mtendaji mkuu brela aanza kazi rasmi

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
Bw. Godfrey Nyaisa (Mwenye tai nyekundu) akisalimiana wadau wa BRELA
alipokua akitembelea Ofisi za Idara na Vitengo mbalimbali baada ya
kuwasili leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es
Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
Bw. Godfrey Nyaisa (Mwenye tai nyekundu) akisalimiana na Mkurugenzi wa
Idara ya Leseni BRELA Bw. Andrew Mkapa mara baada ya kuwasili leo
Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji Bw. Bakari Mketo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa akifafanua jambo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
Bw. Godfrey Nyaisa (Mbele) Akizungumza na Wakurugenzi wa Idara na
Vitengo Mbalimbali BRELA mara baada ya kuwasili leo Januari 23, 2020
BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam.
Na Robertha Makinda – BRELA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
Godfrey Nyaisa amewasili rasmi katika kituo chake kipya cha kazi leo
Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam.
Baada ya kuwasili katika BRELA Ofisi Kuu Bw. Nyaisa amepata wasaa kukaa
kikao kifupi na Menejimenti, kutambulishwa kwa wafanyakazi pia kukutana
na baadhi ya wadau wa BRELA waliokua wakipata huduma kwa siku ya leo.
Katika maneno yake ya utambulisho kwa wafanyakazi wa BRELA amewataka wampe ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii.
“Wafanyakazi wanzangu naomba kwa kipindi hiki tushirikiane ili tuweze
kufanya kazi za serikali ni matumaini yangu kila mmoja atasimama katika
nafasi yake na kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha azma ya Tanzania
ya Viwanda na kuwa nchi ya uchumi wa kati”, alisema Bw. Nyaisa.
Aidha alipokua akizungumza na wadau wa BRELA waliokuwa wakipata huduma
siku ya leo, amewaomba waweze kuwa wavumilivu kwa kwa kipindi hiki
wakati BRELA inajipanga kutoa huduma bora na kuondoa malalamiko
yaliyopo, alibainisha Bw. Nyaisa.
Bw. Nyaisa aliteuliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent
Bashungwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA tarehe 19 Januari, 2020
akichukua nafasi ya Bi. Loy Muhando aliekuwa akikaimu nafasi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *