Watu waliofariki dunia kwa virusi vya corona wafikia 425 nchini china

Idadi ya watu waliofariki dunia kwa ugonjwa unaotokana na virusi vya Corona imefikia 425.


Kabla ya hapo viongozi wa idara ya afya nchini humo walikuwa wametangaza kuwa idadi ya wahanga wa ugonjwa huo ni 360. 

Hata
hivyo ripoti iliyotolewa jana imesema kuwa jumla ya watu elfu 990
wamelazwa katika mkoa wa Hubei na kwamba 576 kati yao wana hali mbaya. 

Virusi
vya Corona viliibuka kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka uliopita
katika soko la vyakula vya baharini la mji wa Wuhan nchini China.


Hata
hivyo mbali na mji huo, virusi hivyo sasa vimeenea katika nchi 18 za
dunia. Hii ni katika hali ambayo mashirika mengi ya ndege likiwemo
Shirika la Ndege la Qata, Air Canada, Air France, Air Seoul, American
Airlines, British Airways, Lufthansa, Turkish Airlines na mengine
kadhaa, yamesimamisha safari zao kuelekea China kutokana na hatari ya
virusi hivyo.