Kaimu
Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bw.Imani Sichalwe akizungumza
na wauzaji wa nyama za mafungu katika Machinjio ya Vingunguti Jijini Dar
es Salaam mara baada ya kutembelea katika maeneo hayo kwaajili ya
kuwaondoa. Wauzaji
wa nyama kwa mafungu wakiwa wamewpanga nyama zao kwaajili ya mauzo
ambapo ni kinyume na utaratibu uliowekwa kwa maana unahatarisha afya kwa
mlaji nyama zinazouzwa kwa njia hizo.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama
Tanzania (TMB) Bw.Imani Sichalwe akiwaelekeza wauzaji mifuko kuwa
haitakiwi kwa kubebea nyama kwa maana yakuwa mifuko mingi inakuwa na
kemikali ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu. Kaimu
Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bw.Imani Sichalwe akishuhudia
uuzaji wa nyama kwa mafungu katika maeneo ya machinjio Vingunguti ambapo
aliwaamuru kuondoka mara moja kwa maana uuzaji wa nyama kwa mafungu
katika maeneo hayo ni hatari kwa afya ya mlaji.
(PICHA NA EMMANUEL MBATILO)
NA EMMANUEL MBATILO. DAR ES SALAAM
Bodi ya Nyama Tanzania imewataka
wauzaji wa nyama kwa mafungu maeneo ya machinji Vingunguti kuacha mara
moja kwa maana unaweza kuhatarisha afya ya mlaji wa nyama hizo kwani
wauzaji hawafuati utaratibu wa uuzaji wanyama.
Akizungumza baada ya kutembelea
maeneo hayo Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bw. Imani
Sichalwe amesema uuzaji wa nyama kwa mafungu kiholela unaweza
kusababisha mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu kwa maana uuzaji wa
nyama hizo uuzwa katika maeneo ya wazi ambayo ni hatari.
“Kuanzia sasa huu uuzaji usitishwe
mara moja, mazingira haya ni hatarishi kuna magari yanapita ule moshi wa
gari ni hatari pia kuna inzi wa chooni pamoja na inzi wanaotoka katika
uchafu wanaweza kusababisha magonjwa kama kipindupindu”. Amesema
Bw.Sichalwe.
Aidha Bw.Sichwale amewataka wauzaji
kwenda katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwaajili ya biashara hiyo
lakini sio maeneo kama haya ya wazi.
“Hapa tunaona kinyesi na mikojo
karibu sana na hapa mnapouzia hizi nyama kwani ninyi hamuoni kama ni
hatari kwa afya, mlipuko kwa mangojwa ukitokea wakwanza kuathirika ni
ninyi ambao hamfuati utaratibu hapa”. Amesema.
Hata hivyo amesema kuwa dhumuni la
Serikali sio kuwakataza watu kufanya biashara bali kuwashawishi
wafanyabiashara kufanya biashara zao katika hali nzuri na kuzingatia
afya kwa mlaji.