Waziri kalemani aagiza wakandarasi kuanza utekelezaji wa mradi wa kumalizia vijiji visivyo na umeme

 

Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na Wakandarasi kutoka
Kampuni 34 ambao wanatekeleza Mradi wa usambazaji umeme Vijijini wa
Awamu ya Tatu, mzunguko wa Pili (hawapo pichani) kilichofanyika leo Mei
25,2021 jijini Dodoma.



Naibu
Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akizungumza wakati wa kikao
na Wakandarasi kutoka Kampuni 34 ambao wanatekeleza Mradi wa usambazaji
umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu, mzunguko wa Pili (hawapo pichani)
kilichofanyika leo Mei 25,2021 jijini Dodoma.



Mkurugenzi
Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini REA, Mhandisi Amos Maganga
akizungumzawakati wa kikao cha Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani na
Wakandarasi kutoka Kampuni 34 ambao wanatekeleza Mradi wa usambazaji
umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu, mzunguko wa Pili (hawapo pichani)
kilichofanyika leo Mei 25,2021 jijini Dodoma.



Baadhi
ya Wasimamizi wa Miradi ya usambazaji umeme vijijini kutoka Wizara ya
Nishati, watendaji wa REA, TANESCO na wakandarasi wa mradi wa
usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili
wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani (hayupo pichani)
kilichofanyika leo Mei 25,2021 jijini Dodoma.wa mwisho kutoka kushoto ni
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi
Jones Olotu.



Baadhi
ya Mameneja wa TANESCO kutoka sehemu mbalimbali nchini pamoja na
Wakandarasi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu,
mzunguko wa Pili wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani
(hayupo pichani) wakati alipofanya kikao na wakandarasi hao jijini
Dodoma.




Na.Alex Sonna,Dodoma


WAZIRI
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaagiza wakandarasi walioshinda
zabuni ya kutekeleza Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya
Tatu Mzunguko wa Pili kuripoti kwa viongozi wa wilaya ambako
wanatekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini pamoja na kuanza
utekelezaji wa Mradi huo mara moja.


Dkt.
Kalemani alitoa agizo hilo leo Mei 25,2021 jijini Dodoma wakati wa
kikao kazi kati ya Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
TANESCO na wakandarasi amesema kuwa Kuna faida nyingi za kuripoti
katika ofisi za wilaya na vijiji ikiwa ni pamoja na kupata uhakika wa
usalama wa rasilimali watu na vifaa vya mradi. Madhara ya kutoripoti ni
makubwa zaidi”


“Baada ya mkutano huu msambae katika maeneo yenu ya kazi mara moja..niwaombe sana muende site
muanze kuchapa kazi” alisema na kuwataka wahakikishe wanaunganisha
umeme kwenye vijiji vyote nchini ambavyo havina huduma ya umeme ndani ya
miezi 18 kuanzia sasa.


Amesema kuwa wakandarasi watekeleze miradi kwa kushirikisha viongozi na
wananchi ili kujenga mahusiano mazuri na watoe kipaumbele kwa kutoa
ajira hasa kazi za vibarua kwa vijana wa vijijini ambako miradi ya
kusambaza umeme inatekelezwa.

Dkt.
Kalemani amewataka wakandarasi kuwaunganishia umeme wananchi ndani ya
siku 14 baada ya kufanya malipo ya kuunganishiwa umeme na wasibague
nyumba za tembe, vibanda vya biashara pamoja na maeneo ya mazizi ya
mifugo kwa wananchi watakaohitaji huduma hiyo.


Aidha Dkt.Kalemani ametoa onyo kwa wakandarasi na mafundi wanaoweka mifumo ya nyaya ndani ya nyumba ‘wiring
ambao sio waaminifu kuacha tabia hiyo mara moja ya kuwatapeli wananchi
na kuwataka REA na TANESCO kuhakikisha kero hiyo haitokei tena katika
miradi ya kusambaza umeme vijijini.

Miongoni
mwa mambo ambayo Waziri amewasisitizia wakandarasi kuyazingatia ni
pamoja na kununua vifaa bora vinavyotengenezwa na viwanda vya ndani ya
nchi na amewataka wenye viwanda kutengeneza vifaa vyenye ubora na kwa
wingi ili kukidhi mahitaji ya miradi ya kusambaza umeme vijijini.


Amesema kutokana na mradi huo kutohusisha ulipaji fidia kwa wananchi
ambao sehemu ya maeneo yao itatumika kupitishia miundombinu ya umeme,
wakandarasi wanapaswa kutumia busara wakati wa ujenzi wa miundombinu
hiyo.

“Mwananchi ana kiwanja chake kidogo, lakini nguzo inatakiwa kuwekwa
katika eneo hilo. 

Utakuta
badala ya nguzo kuwekwa mahali ambapo ataweza kuendelea na shughuli
nyingine katika eneo hilo, mkandarasi anasimika nguzo katikati ya
eneo…naomba mkatumie busara mkapitishe miundombinu ya umeme pasipo
kuathiri matumizi eneo la mwananchi,” amefafanua.

Hata
hivyo, Dkt. Kalemani amesema ili kupunguza hujuma za vifaa na
miundombinu, wakandarasi wanapaswa kuajiri vibarua ambao ni waaminifu na
wawe wa kwanza kulinda vifaa vyao na aliwataka wananchi kuacha kuhujumu
miundombinu ya kusambaza umeme vijijini.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ameahidi
kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati huku akiwataka wasimamizi
wa mradi kuwa vikao kazi na wakandarasi katika maeneo ya miradi na
kuandaa ripoti za vikao hivyo ambazo zitatumika kwa ajili ya maelekezo
ikiwa ni pamoja na kuboresha utekelezaji wa Mradi.

 “Tutajikita zaidi kusimamia mikataba yenu, kuna wengine hamzingatii masharti ya mikataba yenu lazima tukumbushane” amesema. 

 

Naye
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga amewahakikishia
wakandarasi kuwa Serikali inafuatilia malalamiko ya hujuma ya
miundombinu na vifaa katika baadhi ya maeneo na kuwashauri
wawashirikishe viongozi wa vijiji katika ulinzi wa vifaa.

Promoted Content

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore….Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog

Promoted Content

 Bofya Hapa

 Bofya Hapa

TANGAZO

WASILIANA NASI

Name

Email
*

Message
*