Waziri kalemani aridhishwa na utendaji kazi wa wakala wa nishati vijijini (rea)


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani,akizungumza wakati akifunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi
wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo
lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini
uliofanyika jijini Dodoma.



Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen
Byabato,akizungumza na Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO
Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya
usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.



Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba
ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati
akifunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi na
Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini
utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini
Dodoma.



Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa
wakala wa umeme vijijini (Rea) Mhandisi Advera Mwijage,akitoa neno la
shukrani kwa niaba ya washiriki baada ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani kufunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi
na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini
utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini
Dodoma.




Na.Alex Sonna,Dodoma


Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Medard
Kalemani,amesema kuwa, Serikali imeridhishwa na utendaji kazi wa Wakala
wa Nishati Vijijini (REA) na Wizara ya Nishati imekuwa ikijivunia
utendaji kazi wao.


Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati
akifunga kikao kazi cha siku mbili cha kutathimini utekelezaji wa miradi
ya kusambaza umeme vijijini kilichowashirikisha REA na TANESCO.


Dkt. Kalema amewataka REA kulinda
hadhi yao kwa kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme katika maeneo
mbalimbali ambayo hayajafikishiwa huduma ya nishati ya umeme.


“Ndugu zangu mafanikio ya nchi hii
yanategemea REA na TANESCO, vigezo vilivyofanya tuingie kwenye uchumi wa
kati umeme umechangia kwa kiasi kikubwa sana” amesema Dkt. Kalemani.


Dkt.Kalemani amesema kuwa Serikali
imeweka malengo na mipango yake kuhakikisha wananchi kila Kijiji
wanapata nishati bora ya umeme hivyo muhakikishe vijiji vyote vinapata
nishati ya umeme.


”Maeneo ambayo REA imekuwa na
mafanikio ni kufikisha umeme katika vijiji 10,300 sawa na asilimia 87,
kati ya vijiji 12,268 hapa nchini na lengo letu ni kuhakikisha vijiji
vyote vinapata Nishati ya umeme”amesema Dkt.Kalemani


Naye , Naibu Waziri wa Nishati Wakili,
Stephen Byabato,aliwapongeza REA kwa kufanya kazi nzuri ya usambazaji
umeme nchini na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi.


Kwa upande wake Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa REA), Mhandisi Advera Mwijage, amesema kuwa
watahakikisha maagizo yote yaliyotolewa na Waziri wanayafanyia kazi ili
wananchi wote wanufaike na nishati hiyo ya umeme.