Waziri lukuvi afungua mkutano wa matumizi bora ya rasilimali ardhi na uhifadhi wa mandhari za afrika, arusha

Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi (Mb)
akifungua Mkutano wa Kimataifa kuhusu Matumizi Bora ya Rasilimali za
Ardhi katika Mandhari ya Afrika (
African Landscapes Dialogue) unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) jijini Arusha












Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi (Mb)
akifungua Mkutano wa Kimataifa kuhusu Matumizi Bora ya Rasilimali za
Ardhi katika Mandhari ya Afrika (African Landscapes Dialogue) unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) jijini Arusha



Mwenyekiti
wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Fidelis
Mutakyamilwa akimkaribisha Waziri kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano huo.




Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ambaye
ndiye mwenyeji wa Mkutano huo Dkt. Stephen Nindi akitoa maelezo ya
utangulizi kuhusu malengo na matarajio ya mkutano kabla ya kufuguliwa na
Mh. Waziri



Mwakilishi
wa Wizara ya Kilimo kutoka Serikali ya Uholanzi Bw. Hayo Haastra akitoa
maelezo kwa washiriki namna Serikali ya Uholanzi inavyoshiriki kwenye
mijadala ya matumzi ya ardhi katika mandhari mbalimbali za Afrika.



Mkurugenzi wa Eco Agriculture Sara Scherr, akitoa maelezo ya namna taasisi yake ilivyoshiriki katika maandalizi na kufanikisha kufanyika kwa Mkutano huo.



Mwakilishi
kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) Boris Buechler
akizungumza na washiriki kuhusu ushiriki wa Shirika hilo kwenye masuala
mbalimbali ya matumizi ya rasilimali ardhi katika mandhari za Afrika




 Mwakilishi
kutoka Senegal Chimmere Diaw wa African Model Forest Network
akiwasilisha mada ya jinsi ya kusimamamia mandhari jumuishi ya matumizi
ya ardhi




 Bwana
John Recha kutoka programu ya mabadiliko ya Tabianchi akiwasilisha mada
kuhusu upangaji matumizi ya ardhi katika mandhari mbalimbali kwa
kuzingatia Sera na mabadiliko ya tabianchi




 Mkurugenzi
wa Shirika la Solidaridad Afrika Mashariki na kati Rachel Wanyoike,
akiendesha moja ya mijadala kuhusu matumizi ya ardhi katika mandhari
mbalimbali za Afrika





 Washiriki wakifuatilia Mkutano




 Picha ya pamoja ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Matumizi Bora ya Rasilimali za Ardhi katika Mandhari ya Afrika (African Landscapes Dialogue)
(Picha na Fredy Njeje)




Na Mwandishi Wetu, APC BLOG, ARUSHA

Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi, amefungua
Mkutano wa Kimataifa kuhusu matumizi bora ya rasilimali ardhi kwenye
Mandhari mbalimbali za Afrika wenye lengo la kujadili hali halisi na kubadilishana uzoefu katika upangaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi katika Mandhari hizo.






Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Mh. Lukuvi amewapongeza Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kama muandaaji mwenyeji, asasi zisizo za kiseriali za ECO Agriculture Partners pamoja na wadau wengine wote waliofanikiwa kufanyika kwa mkutano huo na Tanzania kuwa mwenyeji kwa mwaka huu.
 
Aidha, Mh. Lukuvi amewataka wadau hao kutoka ndani na nje ya nchi kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kisekta yenye lengo la kuimarisha Mandhari Duniani hasa katika kipindi hiki ambacho mabadiliko ya tabia nchi yanazidi kushamiri na kuathiri uzalishaji na maisha ya binadamu katika maeneo mbalimbali Duniani.

Mkutano huo wa siku nne, unatarajiwa kujadili masuala ya uanzishwaji na utawala wa mandhari, utekelezaji na upangaji wa mandhari kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi, uimarishaji wa biashara, ajira na ujasiriamali katika uchumi wa kijani. 
Masuala mengine ambayo yanatarajiwa kujadiliwa ni pamoja na usimamizi wa wanyamapori na bionuai katika mandhari pamoja na udhamini kifedha, Uwekezaji, haki za miliki na matumizi ya ardhi katika mandhari. 



Inategemewa kuwa, kufanikiwa kwa utekelezaji wa masuala hayo yote katika nchi mbalimbali za Afrika na dunia kwa ujumla itakuwa ni chachu katika kuimarisha uchumi na kuleta maendeleo ya nchi na hatimaye kufanikiwa kwa malengo endelevu ya maendeleo (Sustainable Development Goals)