Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akiwahimiza wawekezaji kuja
kuwekeza Tanzania katika Mkutano wa Kibiashara na Uwekezaji kati nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sweden kwa njia ya mtandao uliofanyika
tarehe 27/04/2021 katika ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali,
Mtumba Dodoma.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akifuatilia kwa makini
majadiliano katika Mkutano wa Kibiashara na Uwekezaji kati nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sweden kwa njia ya mtandao uliofanyika
tarehe 27/04/2021 katika ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali,
Mtumba, Dodoma.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (kulia) na Mkurugenzi
Idara ya Mtangamano wa Biashara ya wizara Bw. Ali Gugu (kushoto)
katikati ni Mtumishi wa Wizara wakiwa katika Mkutano wa Kibiashara na
Uwekezaji kati nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sweden kwa njia ya
mtandao uliofanyika tarehe 27/04/2021 katika ofisi za Wizara zilizopo
Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Kulia) akiwa na Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (katikati) na
Mkurugenzi Idara ya Mtangamano wa Biashara ya wizara Bw. Ali Gugu
(kushoto) katika Mkutano wa Kibiashara na Uwekezaji kati nchi za Jumuiya
ya Afrika Mashariki na Sweden kwa njia ya mtandao uliofanyika tarehe
27/04/2021 katika ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba
Dodoma.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amewahimiza wawekezaji
kutoka Sweden kuja kuwekeza Tanzania kwa kuwa ina fursa na rasilimali
nyingi, hali ya hewa na mazingira mazuri kwa ajili ya biashara na
uwekezaji.
Profesa
Mkumbo aliyasema hayo katika Mkutano wa Kibiashara na Uwekezaji kati
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sweden uliofanyika kwa njia ya
mtandao tarehe 27/04/2021 katika ofisi za Wizara zilizopo Mji wa
Serikali Mtumba, Dodoma.
Akiongea
katika Mkutano huo, Waziri wa Viwanda na Biashara alieambatana na Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb.), alisema Tanzania
itaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Sweden na itaendelea
kutekeleza makubaliano mbalimbali ya ushirikiano wa kibiashara kati ya
nchi hizo.
Akiwahimiza
wawekezaji hao kuja kuwekeza Tanzania, Waziri alisema kuwa Tanzania
inafanya jitihada mbalimbali katika kuboresha mazingira ya biashara na
uwekezaji ikiwemo sera na sheria kupitia utekelezaji wa “Blueprint”,
miundombinu ya usafirishaji nchi kavu,baharini na angani pamoja na
kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa jiji kubwa la kibiashara ifikapo
mwaka 2025.
“Nawasihi
wawekezaji kuja kuwekeza nchini ili kuiwezesha Tanzania kuuza mazao
yaliyoongezwa thamani na si malighafi, pamoja na kubadilishana
teknolojia ya kisasa kati ya Tanzania na Sweden”. Alisema Profesa
Mkumbo.
Aidha,
Profesa Mkumbo aliwahimiza wawekezaji hao kuja kuwekeza katika sekta
mbalimbali Tanzania yenye maliasili nyingi kwa kuzingatia utunzaji wa
mazingira, soko la nchi sita (6) zisizo na bahari zinazohudumiwa na
Bandari za Tanzania na upatikanaji wa Ajira kwa urahisi.
Mkutano
huo kwa njia ya mtandao, ulihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje,
Biashara na Masuala ya Nchi za Nordic wa Sweden, Waziri wa Wizara ya
Ustawi wa Viwanda, Biashara na Ujasiriamali wa Kenya; Waziri wa TEHAMA
na Ubunifu wa Rwanda; Waziri wa Biashara, Viwanda na Ushirika wa Uganda;
Balozi wa Tanzania nchini Sweden; Balozi wa Rwanda nchini Sweden; na
Naibu Amid wa Mabalozi wa Afrika Mashariki nchini Sweden
Wengine
waliohudhuria Mkutano huo ni Mwenyekiti wa Kituo cha Biashara cha
Sweden Afrika Mashariki (SWEACC), Rais wa Kituo cha Biashara, Viwanda na
Kilimo Tanzania (TCCIA), Katibu Mkuu wa Kituo cha Biashara na Viwanda
Uganda; pamoja na Viongozi wengine wanaowakilisha wafanyabiashara na
wenye viwanda kutoka Sweden na nchi za Jumuiya Afrika Mashariki.