WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa nchini wahakikishe
wanasimamia ipasavyo ujenzi wa vyumba vya madarasa vikamilike kwa wakati
ili wanafunzi wote waliochagulia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka
2020 waanze masomo kwa pamoja.

Amesema
lengo la Serikali ni kuhakikisha wanafunzi wote wanaanza kusoma kwa
pamoja kwa sababu wakipishana muda wa kuanza masomo baadhi yao
wanashindwa kufanya vizuri jambo ambalo si sahihi.

Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Desemba 29, 2019) wakati akitoa
taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015/2020 kwenye
mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ruangwa.

Jumla
ya watahiniwa 933,369 sawa na asilimia 98.55 ya waliosajiliwa
walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 na kati yao
watahiniwa 759,737 wamefaulu ambao ni sawa na asilimia 81.50.

Kati
yao wasichana ni 395,738 ambao ni sawa na asilimia 80.87 na
wavulana ni 363,999 sawa na asilimia 82.20. Mwaka 2018
watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 77.72, hivyo kuna
ongezeko la ufaulu kwa asilimia 3.78.

“Wakuu
wa Mikoa hakikisheni vyumba vya madarasa vinakamilika ili wanafunzi
wote waliofaulu waanze masomo kwa pamoja. Kitendo cha wanafunzi
kupishana kuanza masomo kinawafanya waliochelewa kutofanya vizuri katika
mitihani yao.”

Kadhalika,
Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi hao wahakikishe wanasimamia vizuri
elimu kwa watoto wa kike na kuwachukulia hatua watu wote watakaobainika
kuwakatisha masomo iwe kwa kuwaoa, kuwaozoesha au kuwapa ujauzito.

Serikaliimeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike lengo ni
kumuwezesha amalize masomo yake ili aweze kujikwamua kiuchumi na
aondokane na utegemezi, hivyo ni marufuku kuwakatisha masomo.

“Watoto
wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii na Serikali itatoa adhabu
kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto
wa kike iwe kwa kumuoa au kumpa ujauzito.”

Mkuu amesema Serikali inataka kuona idadi kubwa ya watoto wa kike
wanatimiza malengo yao kielimu, hivyo ni lazima wakaondolewa vishawishi
kwa kuboresha mazingira yao ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na kuongeza
idadi ya mabweni.

Wakati
huo huo, Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa
na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo na wilaya
ya Ruangwa ambayo imepewa sh. bilioni 38 kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi ya kimkakati.

Mkuu ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya
Ruangwa kwa kubuni mradi wa kimkakati wa ujenzi wa ghala la kuhifadhia
mazao na pembejeo linalojengwa katika kijiji cha Lipande. Ujenzi huo
unaogharimu sh bilioni 5.45.

Ghala
hilo ambalo limeanza kutumika lina uwezo wa kuhifadhi tani 20,000
litaiwezesha halmashauri kujiongezea mapato ya ndani na kusaidia
kupunguza utegemezi kutoka Serikali Kuu na wafadhili. Pia litapunguza
gharama za usafirishaji wa korosho walizokuwa wanatozwa wakulima wakati
wa kusafirisha mazao.

katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano miradi
mingi ya kimkakati imetekelezwa nchini ambayo ni pamoja na ujenzi wa
reli ya kisasa (SGR), upanuzi wa bandari za Mtwara, Dar es Salaam na
Tanga, uboreshwaji wa viwanja vya ndege, ununuzi wa rada na ununuzi wa
ndege mpya.

Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano tangu ilipoingia madarakani
mwaka 2015, kipaumbele chake kilikuwa ni kukuza kiwango cha uchumi
kutoka cha chini kwenda cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia sekta ya
viwanda.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, DESEMBA 29, 2019.