Waziri mkuu majaliwa arejea nchini


Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza  na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kwenye
uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ,Oktoba 29, 2019
wakati  alipowasili nchini akitoka nchini  Azerbaijan ambako
alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika mkutano wa Nchi
zisizofungamana na upande wowote ulifanyika jijini Baku.


(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, Ieo
Oktoba 29, 2019 amerejea nchini akitoka Baku nchini, Azerbijan ambako
alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa 18 wa
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi zisizofungamana na upande wowote.

Baada ya kuwasili katika
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Waziri Mkuu amepokelewa
na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson Mwansasu pamoja na viongozi
wengine wa Mkoa wa Dar es salaam.

Awali, Mheshimiwa Majaliwa
alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Mataifa ya Afrika na Urusi uliofanyika katika mji wa
Sochi nchini Urusi.