Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akizungumza na
Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania
Bw.Abdullahi Baba aliyemtembelea ofisini kwake leo Januari 29,2021
jijini Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akimsikiliza
Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania
Bw.Abdullahi Baba wakati wa mazungumzo ofisini kwake leo Januari 29,2021
jijini Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akiwa katika picha
ya pamoja na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini
Tanzania Bw.Abdullahi Baba mara baada ya mazungumzo ofisini kwake leo
Januari 29,2021 jijini Dodoma
Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akizungumza na wazalishaji
wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza
uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma
Baadhi
ya wazalisha wa Sukari Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey
Mwambe,wakati wa kikao cha wazalishaji wa Sukari nchini ambapo
amesikiliza changamoto zao na kuahidi kuzitatua na kuongeza uzalishaji
wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma
Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akisisitiza jambo zaidi
wakati wa kikao na wazalishaji wa Sukari nchini pamoja na kusikiliza
changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo
Januari 29,2021 jijini Dodoma
Afisa
Mtendaji Mkuu Utawala TPC Bw.Jaffari Ally akielezea jambo kwa Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe(hayupo pichani) wakati wa kikao
cha wazalishaji wa Sukari nchini ambapo amesikiliza changamoto zao ili
kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini
Dodoma
Mkurugenzi
Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania Prof.Kenneth Bengesi,akizungumza kwenye
kikao cha wazalishaji wa Sukari nchini ambapo Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe ameahidi kuzitatua changamoto hizo ili
kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini
Dodoma
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na wazalishaji wa
Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza
uzalishaji na kuhakikisha Sukari inapatikana kwa urahisi wakati wote
nchini.
Akizungumza
na na wazalishaji hao leo Janauari 29,2021 jijini Dodoma Mhe.Mwambe
amesema kuwa Serikali inalenga kuongeza uzalishaji wenye tija kwa
kutumia teknlojia na miundombinu ya kisasa ya umwangiliaji.
”Leo
nimekutana na nyie kwa leongo la kujifunza na kujua changamoto
mlizonazo katika uzalishaji wa sukari nchini na waahidi tutazifanyia
kazi”amesema Mhe.Mwambe.
Hata
hivyo Mhe.Mwambe amewatoa wasiwasi wazalishaji hao kuwa Serikali
itashughulikia changamoto hizo ili kuleta maendeleo na kuongeza
uzalishaji zaidi nchini .
Awali
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na kufanya
mazungumzo na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini
Tanzania Bw.Abdullahi Baba.