Waziri wa kilimo: tunataka mbegu bora za mazao ya kilimo zizalishwe nchini

Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga ameagiza wataalam wa wizara na taasisi nchini
kutumia utaalam na uwepo wa fursa nzuri ya umwagiliaji kuzalisha mbegu
bora kwa matumizi ya wakulima.

Amesema
kauli hiyo leo Jijini Dodoma wakati alipofungua kikao kazi cha
Menejimenti ya wizara,taasisi na bodi za mazao  zilizo chini ya wizara
ya Kilimo 
Hasunga
amesema Tanzania haina haja ya kutegemea mbegu za mazao toka nje wakati
ina eneo linalofaa kwa uzalishaji la kutosha na wataalam wabobezi
kwenye sekta ya uzalishaji mazao ya kilimo .
“Tunataka
mbegu zizalishwe kipindi cha kiangazi kupitia kilimo cha
umwagiliaji,ili wakati wa mvua wakulima wapande wala sio muda wa
kuzalisha mbegu” alisema Hasunga
Waziri
Hasunga ametoa takwimu kuwa kwa sasa Tanzania inatumia tani 186,000 za
mbegu ambapo uzalishaji ndani ya nchi ni chini ya tani 71,000 kwa mwaka
hali inayosababisha kuendelea kutegemea mbegu zinazozalishwa nje.
Ameitaja
changamoto ya upungufu wa mbegu za miche ya chai,korosho ,michikichi,
kahawa , mihogo  na jamii ya mikunde hivyo kuchangia ukuaji mdogo wa
tasnia za mazao hayo
Waziri
huyo wa kilimo aliwaambia watendaji na watalaam wa wizara yake kuwa
tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
ameagiza kuwa nchi iwe na mkakati maalum wa kuongeza uzalishaji kwa
kutumia kilimo cha umwagiliaji.
Hasunga
amesema katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli,wizara yake tayari
imeagiza taasisi zake kutumia fursa ya umwagiliaji kuongeza uzalishaji
mbegu nchini.
Amesema
Tanzania ina eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji hekta milioni
29.4 ambapo zinazomwagiliwa hadi sasa ni hekta 475,000 tu hivyo wataalam
wahakikishe mbegu zinazalishwa kwa wingi muda wote wa mwaka.
Wakati
huo huo Waziri Hasunga ameonya dhidi ya kuongezeka kwa mbegu,mbolea na
viuatilifu visivyo bora(fake) hali inayowaumiza na kusababisha hasara
kwa wakulima nchini.
“Madawa
na viuatilifu ambayo hayaruhusiwi kutumika yapo mengi sana.Hata mimi
(Waziri) mwaka jana nilipigwa madawa yasiyo na ubora katika shamba langu
Songwe na magugu hayakufa “ alitoa mfano Waziri Hasunga.  
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof.Siza Tumbo
amemhakikishia Waziri kuwa watendaji wa wizara na taasisi zake
wataendelea kutekeleza maagizo ya serikali muda wote ili tija katika
uzalishaji mazao nchini iongezeke.
Kikao
hiki cha Menejimenti ni cha nne tangu Waziri Hasunga alipoteuliwa
kuongoza wizara hiyo mwaka 2018 ambapo taarifa za utendaji kazi
hujadiliwa pamoja na kuweka mpango wa utekelezaji kwa nusu ya pili ya
mwaka 2020 iliyobakia.
Wizara
ya kilimo ina bodi za mazao na taasisi zinazojitegemea jumla 22 ambapo
wakurugenzi wakuu na wenyeviti wake wa bodi  wote wanashiriki kikao hiki
cha Waziri wa Kilimo mwaka huu.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Kilimo