Waziri wa Mambo ya Ndani, George
Simbachawene (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi
Jinai, David Elias (kushoto) akimueleza kuhusu uchunguzi wa kimaabara wa
dawa za kulevya unavyofanyika kwa kutumia mitambo ya kisasa katika
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye Maadhimisho ya Siku
ya Dawa za Kulevya Duniani ambapo kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa
Nyerere Square, mkoani Dodoma leo. Katikati ni Kamishna Jenerali wa
Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila
Kusaya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za
Sayansi Jinai, David Elias (kushoto) wakati akimuonesha takwimu za
uchunguzi wa dawa mbalimbali za kulevya zilizochunguzwa katika maabara
za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miaka
sita wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani
leo tarehe 26 Juni, 2021 ambapo Waziri Simbachawene alishiriki kwa
niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambapo kitaifa yamefanyika katika
Uwanja wa Nyerere Square, mkoani Dodoma. Katikati ni Kamishna Jenerali
wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila
Kusaya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene (kulia), akisaini kitabu cha Wageni baada ya
kutembelea banda la Mamlaka wakati wa kilele cha Maonesho ya Maadhimisho
ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambapo kitaifa yamefanyika mkoani
Dodoma katika Uwanja wa Nyerere Square leo tarehe 26 Juni, 2021.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt.
Fidelice Mafumiko (kushoto) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Mamlaka
ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya
(kulia).
Mkemia Mkuu wa Serikali, (katikati)
na Msajili wa Baraza la Wafamasia, Elizabeth Shekalaghe (kulia)
wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti
Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya (kushoto) wakati wa Maadhimisho
ya Siku ya Dawa za Kulevya jijini Dodoma leo.
Mkemia Mkuu wa Serikali, (wa pili
kulia) akimsikiliza Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai wa Mamlaka ya
Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Betha Mamuya (kulia) mara
baada ya kutembelea banda la Mamlaka katika Maadhimisho ya Siku ya Dawa
za Kulevya yaliyofanyika leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Huduma za Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali, David Elias.
Watumishi wa Mamlaka walioshiriki Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya jijini Dodoma.
Mtumishi wa Mamlaka, Muhsin Kilonzo
(kulia) akiongea na mmoja ya mdau aliyetembelea banda la Mamlaka kwenye
Maonesho ya Maadhimisho ya siku ya Dawa za Kulevya yaliyohitimishwa leo
katika Uwanja wa Nyerere Square, Dodoma.
Kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, George Simbachawene, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Khamis Hamza Chilo na Kamishna wa Mamlaka ya Kupambana na
Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya, wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (hayupo pichani)
walipotembelea banda la Mamlaka katika Maonesho ya Maadhimisho ya Siku
ya Dawa za Kulevya yaliyofikia kilele leo jijini Dodoma.