Wft-trust na c4c wawasilisha tathmini matokeo ya utafiti juu ya ukatili katika halmashauri ya wilaya ya shinyanga

Mtafiti wa haki za wanawake na watoto kutoka taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru (TICD)  na Citizen for Change C4C Bwana Mathias Mkude akizungumza kwenye kikao hicho leo Jumatano Agosti 16,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga.

Na Hyasinta Ludovick, Mapuli Misalaba – Shinyanga

Wanawake ni kundi linalotajwa kukumbatia mifumo dume
inayo sababisha kuendelea kwa vitendo vya ukatili katika jamii.

Hayo yamebainishwa na mtafiti wa haki za wanawake na
watoto kutoka taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru (TICD)  na Citizen for Change C4C Bwana Mathias Mkude
,kwenye kikao cha kutoa matokeo ya utafiti wa kubaini visababishi vya ukatili
dhidi ya wanawake na watoto.

Mkude amesema Utafiti huo umebaini kuwa wanawake ni
miongoni mwa watu wanaoendeleza  mifumo
hiyo hasa katika ngazi ya familiya hali inayochangia kuendelea kuwepo kwa
vitendo  vya ukatili .

“Matokeo
ya utafiti huu yanaonyesha kwamba mifumo isiyo rasmi inafanya kazi kwa nafasi
ya kipee zaidi ya mifumo rasmi tulipita kwenye nyumba takribani zaidi ya elfu
moja lakini katika hilo tulijaribu  kuangalia ni watu gani wanafuatwa zaidi pale
watu wanapokutana na suala la ukatili kila kata walitajwa watu watatu na
tulipata watu 54 na watu 50 walikuwa kwenye mfumo usiorasmi na wanne ndiyo
walikuwa kwenye mfumo rasmi’.

“Tumegundua
pia pamoja na kuwepo kwa matokeo ya ukatili wanawake kwa kiasi kikubwa ndiyo
waendelezaji wa mifumo inayopelekea ukatili yaani mfumo dume hata mama kwenye
ngazi ya familia anaona umuhimu wa mtoto wa kiume kuliko mtoto wa kike kwahiyo
wanaamini kwamba ili uwe mwanaume lazima uwe mtu mwenye nguvu”.

“Lakini
jamii iliweza kupendekeza njia saba ikiwemo kurudisha taratibu na kanuni  zile za  kimila zilikuwa zinawaweka pamoja kujadili
pamoja na kutoa mambo ya pamoja lakini pia wamezungumza umuhimu wa kuwa na
sheria ndogondogo ambazo zinazingatia katiba ya Nchi maana asilimia kubwa
wanatumia sungusungu lakini hawa sungusungu wasipotengenezewa sheria za
kuzifuata wakati mwingine inapelekea ukatili kwa watu wanaowapa adhabu”.amesema
Mkude

Kwa upande wake mratibu wa Mfuko wa
Ruzuku wa Wanawake Tanzania Mkoani Shinyanga (WFT-Trust) Glory Mbia

amesema utafiti huo umefanyika ndani ya  Miaka miwili (2) katika Halmashauri ya Wilaya
ya Shinyanga.

Afisa Miradi mwandamizi anaye shughulikia utetezi wa
haki za watoto kutoka WFT Tanzania  Neema
Msangi amebainisha malengo na majukumu ya mfuko huo katika kuyawezesha mashirika
madogo na kwamba hatua hiyo ni njia ya kufikia malengo katika utetezi wa haki
za wanawake na watoto.

“WFT
ni mfuko wa ufadhiri ambao ulianzishwa toka mwama 2008 ukiwa na malengo makubwa
ya kuangalia ufikiwaji wa haki za wanawake, wasichana na watoto kwa kuangalia
upatikanaji wa rasilimali”.

“Lengo
ni kuyafikia makundi au mashirika madogo ambayo yapo kwenye ngazi ya jamii ambao
wanashindwa kufikia fund ambazo zipo juu tukaona tuwe na mfuko wa kuwawezesha mashirika
ili kuweza kufikia malengo ya utetezi kwa wanawake, wasichana na watoto”
amesema
Neema.

“Tume
hakikisha jamii inashiriki katika zoezi zima la utafiti huu lakini tumeweze
kuona familia inakaa pamoja na watoto, wanawake wanasimama kwenye mikutano na
kuongea kwa ujasili na kuchangia hoja ambazo zinaleta  maendelea kwenye jamii lakini pia atumweza kuona
kunaongezeko la idadi ya kesi ambazo zimekuwa zikitolewa taarifa na taarifa
hizi tumekuwa tukizifuatilia kwenye dawati la jinsia na watoto na kwa takwimu
ambazo tumekuwa tukizipata ni kila mwaka kunakuwa na ongezeko la kesi hii ni
kuonyesha kwamba jamii imenza kubadilika na kuona umuhimu wa kuripoti”.
amesema
Neema

Msimamzi wa
Rasilimali,utafiti na mawasiliano wa Mfuko wa Rusuku wa Wanawake Tanzania(WFT-Trust),Carol
Mango anasema zoezi la utafiti wa vitendo vya ukatili Halmshauri  ya
wilaya ya Shinyanga lilikuwa ni muhimu ili kuelewa uhalisia wa tatizo la
vitendo vya ukatili na kupata majibu yanayoweza kusaidia kutokomeza ukatili kwa
kushirikisha  jamii yenyewe.

Utafiti huo
ulifanyika kwa miaka miwili kwa kuhoji watu wapatao 1264 kwa makundi mbalimbali
ndani ya Halmashauri  ya wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na shirika
la Citizens  for Change.

Amesema
utafiti huo uliona mambo 9 kwa yanayoweza kujadiliwa na wadau na kutoa maoni
yao ambapo pia amesema zipo changamoto katika utafiti huo ikiwa ni kuchukua
muda mrefu katika kupambana na ukatili ndani ya  jamii.

“Mambo 9 yalibainika ni pamoja
na msaada wa mifumo isiyo rasmi una aminika na kufanya kazi,sheria za
jamii   zina athiri mfumo rasmi,watu katika mfumo rasmi kuona ukatili
ni watu wengine ,wanawake ni walinzi wa mila na destu katika jamii,wanawake na
watoto wanahitaji mabadiliko,wawakilishi wa serikali ngazi ya kata
hawashughuliko ukatili,kuelewa ukatili lazima uelewe nguvu ya mamlaka katika
jamii na jamii inaweza kubadilika na kutegemeza mbinu zake wenyewe na wanaweke
chanzo cha kuendeleza mila na desturi zinachochea ukatili”.
amesema Mango

Akizungumza mgeni rasmi katika kikao
hicho
 cha kuhakiki na kujadili matokeo ya utafiti
(Research Solution  Summit  in Shinyanga) masuala ya ukatili 
uliyofanyika  katika  Halmashauri  ya wilaya ya Shinyanga 
, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa
Mboje amewapongeza na kuwashukuru WFT – Trust kwa kutoa Ruzuku na kutekeleza
miradi ya kupinga ukatili.

Amesema  katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga hali
miradi hiyo imesaidia kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii huku akiomba
kuendelea kutekeleza  miradi  ili kutokomeza kabisa ukatili.

Baadhi ya  wadau
mbalimbali walioshiriki kikao hicho wamepokea huku wakiipongeza WFT – Trust kwa
hatua nzuri waliyofikia katika utafiti Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
ambapo wameahidi kuendelea kuunga mkono jitihada hizo ili kutokomeza mila na
destiri kandamizi zilizopo kwenye jamii.

Kikao cha kutoa matokeo ya utafiti wa kubaini
visababishi vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kilichoendeshwa na taasisi
ya Citizen for Change kwa ufadhili wa mfuko wa ruzuku wa wanawake Tanzania WFT –
Trust kimefanyika kwenye ukumbi wa Karena Hoteli uliopo Halmashauri ya Manispaa
ya Shinyanga.

Mtafiti wa haki za wanawake na watoto kutoka taasisi
ya maendeleo ya jamii Tengeru (TICD)  na
Citizen for Change C4C Bwana Mathias Mkude akizungumza kwenye kikao hicho leo Jumatano
Agosti 16,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa
Wanawake Tanzania Mkoani Shinyanga Glory Mbia
akizungumza
kwenye kikao hicho leo Jumatano Agosti 16,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel
mjini Shinyanga.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa
Wanawake Tanzania Mkoani Shinyanga Glory Mbia
akizungumza
kwenye kikao hicho leo Jumatano Agosti 16,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel
mjini Shinyanga.

 Kikao cha kutoa matokeo ya utafiti wa kubaini visababishi vya ukatili
dhidi ya wanawake na watoto kilichoratibiwa na WFT –Trust kwa kushirikiana na
C4C kiliendelea leo Jumatano Agosti 16,2023 katika ukumbi wa Karena Hotel mjini
Shinyanga.