Ziara ya katibu wa smaujata kanda ya ziwa bwana hashim omary atoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi, shule ya sekondari ngokolo, shule ya msingi little treasures na wananchi manispaa ya shinyanga

 Na Mapuli
Misalaba, Shinyanga

Katibu wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa
jamii Tanzania (SMAUJATA) Kanda ya ziwa Bwana Hashim Omary amewataka wananchi
wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine
katika juhudi za kupinga ukatili wa kijinsia.

Ameyasema hayo leo wakati akitoa elimu ya ukatili
kwa  wanafunzi, wananchi wakiwemo
walengwa  wa Tasaf wa mtaa wa Dome kata
ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ambapo leo
ametembelea shule ya sekondari Ngokolo, shule ya msingi Little Treasures
ikiwa  ni sehemu ya maadhimisho ya siku
16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Bwana Hashim Omary Ramadhan pamoja na mambo mengine amewasisitiza
wananchi kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia,lakini pia  amewataka viongozi kuepuka rushwa katika
utekelezaji wa majukumu yao.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila
Kisendi amewakumbusha wazazi na walezi kuwajibikia jukumu la kuwalinda watoto
dhidi ya ukatili.

Kwa upande wake Mwenyekiti idara ya maadili SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi
Bwana Solomon Najulwa (Cheupe) amesema serikali ya mtaa huo imeendelea kuchukua
hatua dhidi ya watu wanaobainika kufanya ukatili.

Naye katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel
Kapaya amesema kampeni hiyo itaendelea kutoa elimu ya ukatili katika maeneo
mbalimbali huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kuibua na kutokomeza
ukatili unaoendelea kwenye jamii

Leo katibu wa SMAUJATA kanda ya ziwa Bwana Hashim
Omary

leo ametembelea shule ya sekondari Ngokolo, shule ya
msingi Little amefanya ziara ya siku moja ambapo ameungana na viongozi
mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga kutoa elimu ya ukatili ambapo ametembelea shule
ya sekondari Ngokolo, shule ya msingi Little Treasures pamoja na kwamba
viongozi wametoa elimu ya ukatili wanafunzi, wananchi wakiwemo walengwa  wa Tasaf wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi
Manispaa ya Shinyanga.

Ziara hiyo pia imekwenda sanjari na maadhimisho ya
siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo viongozi wa SMAUJATA
wamewashukuru viongozi wa serikali Mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano
wanaoendelea kuupata katika kupambana na ukatili.

Viongozi hao wamemshukuru mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mhe. Christina Mndeme, mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, Afisa
maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale pamoja na viongozi wengine
wa serikali.

Aidha viongozi hao wa SMAUJATA wamesema wataendelea
kuunga mkono juhudi za serikali katika kuchochea maendeleo ambapo wamempongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea
kutambua juhudi za kampeni ya SMAUJATA katika kupambana na uhalifu kwenye
jamii.

Pia viongozi hao wamesema wataendelea kutekeleza maono
ya Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt.
Dorothy Gwajima pamoja na Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Shujaa Sospeter Bulugu
katika kutokomeza ukatili Nchini.

SMAUJATA ni kampeni huru ya kupinga ukatili Nchini
ambayo ilianzishwa na Shujaa Sospeter Bulugu kwa kushirikiana na Waziri Dorothy
Gwajima ambapo kampeni hiyo inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya
maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.

 

Katibu wa SMAUJATA Kanda ya ziwa Bwana Hashim Omary na
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wakizungumza na katibu wa Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga baada ya kusaini kitabu cha wageni leo Jumanne Disemba 5,2023.



Viongozi wa SMAUJATA baada ya kuwasili katika shule ya
msingi Little Treasures iliyopo Manispaa ya Shinyanga.